RAIS KIKWETE AWAAPISHA MNADHIMU MKUU WA JWTZ NA MKUU WA JKT IKULU JIJINI DAR

Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akimwapisha Luteni Jenerali Samuel Albert Ndomba (kulia) kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika viwanja vya Ikulu leo jijini Dar es salaam. Meja Jenerali Ndomba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Luteni Jenerali Abdulrahaman Shimbo aliyestaafu utumishi jeshini kwa Umri.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Dkt. Jakaya Kikwete akimwapisha Meja Jenerali Raphael Mugoya Muhuga (kulia) kuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) leo Ikulu jijini Dar es salaam.

Rais Dkt. Jakaya Kikwete (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Jenerali Devis Mwamunyange (kushoto) na maofisa wa Jeshi Luteni Jenerali Samuel Ndomba, Mnadhimu Mkuu wa JWTZ (wa tatu kutoka kushoto) na Meja Jenerali Raphael Mugoya Muhuga mkuu wa JKT walioapishwa leo Ikulu jijini Dar es salaam.

Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Wizara ya Ulinzi na Maofisa wa JWTZ na Jeshi la Kujenga Taifa. 

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Devis Mwamunyange (kushoto) akimweleza jambo Rais Dkt. Jakaya Kikwete (kulia) katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam.Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki (katikati).

Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Luteni Jenerali Samuel Albert Ndomba akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kuapishwa.

Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kulia) akiwaeleza jambo viongozi wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali Saidi Mwema (wa pili kulia) na Kamishina wa Oparesheni wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja . Kulia ni Mkuu wa Majeshi Jenerali Devis Mwamunyange.

Rais Dkt. Jakaya Kikwete akifurahia jambo na Maofisa Waandamizi Wanawake wa JWTZ. Kushoto ni Meja Jenerali Lilian Kingazi  na Meja Jenerali Grace Mwakipunda (kulia). Picha na Aron Msigwa – MAELEZO

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.