RASIMU YA UDHIBITI DAWA BANDIA KATIKA NCHI ZA AFRIKA YAJA

 NA   MAGRETH  KINABO- MAELEZO 
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Chakula na Dawa(TFDA,  Haiiti Sillo  amesema kwamba  kamati maalum inayoaandaa  rasimu za awali   ya mifumo wa kuoanisha  usajili wa dawa  katika nchi za Afrika Mashariki(EAC)  imeshaanza kazi  hiyo ambayo inatarajiwa kukamilika  kipindi cha miaka  miwili ijao.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi huyo  wakati akizungumza na waandishi wa habari  katika mkutano wa Ushirikiano wa wafanyabiashara wa  kutoka nchini China na Tanzania  kuhusiana na kampuni hizo uliofanyika kwenye hoteli ya Hyatt Regency, Kilimanjaro jijini Dares Salaam.
Mkutano huo  wenye lengo la kutoa elimu kwa wanaotaka  wafanyabiashara hao kutoka nchini China wanaotaka kuwekeza katika sekta hiyo.
“Nchi za EAC zinategemee dawa nyingi kutoka nje . Rasimu hiyo itasaidia kuongeza ushirikiano wa kudhibiti  dawa bandia kwa pamoja,” .  utaratibu huu utakuwa na msharti  yanayofanana katika nchi zote ,alisema  Sillo.
Alisema mifumo hiyo itasaidia kupunguza gharama za usajili wa dawa na kuwezesha wananchi kupata dawa zilizo bora na uhakika.
 Sillo  aliwataka waombaji wa kusajili kampuni za utengenezaji dawa na vifaa tiba kuaandaa maelezo  yanayotosheleza  katika kukidhi  viwango vya  ubora na usalama wa bidhaa hizo ili kuepusha ucheweleshaji wa usajili huo.
 “ Changamoto kubwa tunayokabiliana nayo ni  waombaji wa usajili wa kampuni hizo kutokidhi viwango vya ubora na usalama wa bidhaa hizi. Hivyo ninapenda kuchukua nafasi hii kuwataka waombaji  wahakikishe kuwa kabla ya kuwasisilisha maombi ya usajili wahahakikishe maelezo yao yanajitosheleza,” alisema.
Alizitaja changamoto nyingine ni kuwa kutokuwepo kwa watafiti wa kutosha kutathimini ubora na usalama wa dawa , hata hivyo alisema  suala hilo wanalifanyia kazi ili kuongeza rasilimali watu ya kutosha. Changamoto nyingine ni kutokuwepo kwa ripoti za kuonyesha dawa zilizoleta matatizo kwa watumiaji  kutoka kwa watoa huduma za afya  na watengenezaji wa dawa hizo.
Awali akifungua mkutano huo kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya , Regina Kikuli Sillo aliwataka wafanyabiashara hao kuunda mtandao utakaowasaidia kubadilishana  uzoefu katika sekta hiyo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.