*SERENGETI BOYS YAENDELEA KUJINOA


Timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) inaendelea vizuri na kambi ya mazoezi katika mikoa ya Mbeya na Njombe ambapo leo jioni (Septemba 16 mwaka huu) itacheza mechi ya kirafiki mjini Makambako na timu ya Manispaa.
 
Serengeti Boys ambayo iko chini ya Kocha Jakob Michelsen na msaidizi wake Jamhuri Kihwelo imeshacheza mechi nne mkoani Mbeya. Imecheza mechi hizo dhidi ya Tanzania Prisons, Mbozi United, Mbeya City na Kombaini ya Kyela na kupoteza moja tu.
 
Baada ya mechi ya leo, kesho (Septemba 17 mwaka huu) itacheza mechi ya mwisho mkoani Njombe dhidi ya Kombaini ya Makambako na kurejea Dar es Salaam siku inayofuata kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kabla ya mechi dhidi ya Misri.
 
Mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya pili kuwania tiketi ya kucheza fainali za Afrika kwa vijana zitakazofanyika Machi mwakani nchini Morocco itachezwa Oktoba 13 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
 
MECHI YA SIMBA, LYON YAINGIZA MIL 67/-
Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara kati ya Simba na African Lyon iliyochezwa jana (Septemba 15 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 67,793,000.
 
Washabiki 11,505 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambapo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000. Kila timu ilipata sh. 14,603,263.47 wakati asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyokatwa ni sh. 10,341,305.08.
 
Mgawo mwingine umekwenda kwa msimamizi wa kituo sh. 20,000, posho ya kamishna wa mechi sh. 114,000, mwamuzi wa akiba sh. 70,000, et iti.sh. 3,175,000, vishina kwenye tiketi (attachments) sh. 345,150, maandalizi ya uwanja (pitch preparation) sh. 400,000 na Wachina (stadium technical support) sh. 2,000,000.
 
Umeme sh. 300,000, ulinzi na usafi uwanjani sh. 2,350,000, Kamati ya Ligi sh. 4,867,754.49, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,920,652.69, uwanja sh. 4,867,754.49, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,947,101.86, gharama za mchezo sh. 4,867,754.49.
 
Nayo mechi ya ligi hiyo kati ya Tanzania Prisons na Yanga iliyochezwa jana (Septemba 15 mwaka huu) Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya imeingiza sh. 50,435,000.
 
112 WASHUHUDIA MECHI YA JKT RUVU v RUVU SHOOTING
Watazamaji 112 ndiyo waliokata tiketi kushuhudia mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya JKT Ruvu na Ruvu Shooting iliyofanyika jana (Septemba 15 mwaka huu) Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
 
Mapato yaliyopatikana katika mechi hiyo ambapo viingilio vilikuwa sh. 3,000 na sh. 10,000 ni 340,000. Mgawo ulikuwa kama ifuatavyo; kila timu sh. 29,465.87, asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 51,864.40, maandalizi ya uwanja sh. 100,000 na tiketi sh. 89,916.
 
Kamati ya Ligi sh. 9,821.95, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 5,893.17, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 3,928.78, gharama za mchezo sh. 9,821.95 na uwanja sh. 9,821.95.
 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI