SIMBA NA YANGA KUCHEZA USIKU TAIFA OKTOBA 3 LIVE SUPER SPORT DUNIA NZIMA

Simba SC

Na Prince Akbar
MECHI ya kwanza ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baina ya watani wa jadi, Simba na Yanga itakayopigwa Oktoba 3, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam itachezwa kuanzia Saa 1:00 usiku na kuonyeshwa moja kwa moja na kituo cha Televisheni cha SuperSport.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba hiyo itakuwa moja kati ya mechi tano za Ligi Kuu zilizobatizwa jina Super Weekend katika mzunguko wa kwanza, ambazo zote zitaonyeshwa moja kwa moja na SuperSport, zikianza kati ya saa 1:30 jioni na saa 1:00 usiku.
Mechi nyingine ni za Septemba 28 mwaka huu kati ya Azam na JKT Ruvu itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 1:00 usiku, Simba na Tanzania Prisons Septemba 29 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 11:00 jioni, Yanga na African Lyon Septemba 30, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 11:00 na Ruvu Shooting na Mtibwa Sugar Oktoba 1, Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam kuanzia saa 10:30 jioni.
Yanga SC

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*