Taarifa Ya TFF Kwa Vyombo Vya Habari

                            Release No. 156 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Septemba 27, 2012 MECHI ZA SUPER WEEKEND KUANZA KESHO

 Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom inaingia raundi ya nne kesho (Septemba 28 mwaka huu) kwa mechi za Super Weekend ambazo zitaoneshwa moja kwa moja (live) na kituo cha televisheni cha SuperSport cha Afrika Kusini. Mechi ya kwanza ambayo itachezwa kesho itakuwa kati ya Azam na JKT Ruvu Stars. Mechi hiyo itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam itaanza saa 1 kamili usiku kwa viingilio vya sh. 3,000 mzunguko, sh. 5,000 kwa VIP C na VIP B wakati VIP A kiingilio kitakuwa sh. 10,000.

 Jumamosi (Septemba 29 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya Simba na Tanzania Prisons itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 11 kamili jioni. Yanga na African Lyon zitapambana Jumapili (Septemba 30 mwaka huu kwenye uwanja huo huo kuanzia saa 11 kamili jioni. 

 Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam wenyewe utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Ruvu Shooting na Mtibwa Sugar itakayochezwa Oktoba 1 mwaka huu kuanza saa 10.30 jioni. Mechi ya mwisho ya Super Weekend itachezwa Oktoba 3 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ikizikutanisha Yanga na Simba kuanzia saa 1 kamili usiku. 

 RAMBIRAMBI MSIBA WA ERASTO ZAMBI Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Katibu Mkuu mstaafu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Erasto Zambi kilichotokea jana (Septemba 26 mwaka huu) jijini Dar es Salaam kutokana na maradhi. 

Zambi ambaye anatarajiwa kuzikwa Jumapili (Septemba 30 mwaka huu) kabla ya kuwa kiongozi TOC, kwa muda mrefu alikuwa mwalimu wa michezo katik Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ambapo wanamichezo wengi hasa waliokuwa wanafunzi katika chuo hicho wamepita kwake. Msiba huo ambao uko nyumbani kwake Ubungo Kibangu, Dar es Salaam ni pigo kwa familia ya Zambi, TFF na wanamichezo kwa ujumla nchini kutokana na mchango na mawazo aliyotoa kwa shirikisho wakati akiwa kiongozi wa TOC. 

TFF inatoa pole kwa familia ya Zambi, jamaa na marafiki na kuwataka kuwa na uvumilivu katika kipindi hiki cha msiba huo mzito. Mungu aiweke roho ya marehemu Zambi mahali pema peponi. Amina Boniface Wambura Ofisa Habari Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Reactions::

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*