UGANDA KUIVAA TANZANIA KUFUZU CHAN 2014 'SAUZ'

Rais Yoweri Museveni wa Uganda, kushoto akipiga danadana mbele ya nyota wa timu ya taifa ya Uganda The Cranes katika moja ya ziara zake kwenye kambi ya timu hiyo

CAIRO, Misri

KWA mara ya pili, timu ya taifa ya Uganda ‘The Cranes’ imejikuta ikipanga na majirani zao timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ katika michuano ya kuwania kufuzu Mataifa Afrika kwa Nyota wa Ndani (CHAN 2014.

Ratiba hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Hicham El Amrani Makao Makuu ya shirikisho hilo jijini hapa juzi Alhamisi.

Ratiba ya raundi ya awali, raundi ya kwanza nay a pili ya michuano hiyo pia ilitolewa katika sherehe hizo za upangaji ratiba, ambapo jumla ya timu 15 zitakazofuzu zitaungana na wenyeji wa CHAN 2014 Afrika Kusini kwa fainali hizo zilizoanza mwaka 2009.

Hii ni mara ya pili kwa Uganda ambayo inanolewa na Bobby Williamson kuumana na Tanzania katika kuwania kufuzu fainali hizo, mara ya kwanza ikiwa ni kuelekea fainali za mwaka 2011, zilizofanyika nchini Sudan.

Hata hivyo, kikosi cha Bobby hakikuwa na makali stahili baada ya kuing’oa Tanzania, kwani ilipofuzu huko ilijikuta ikiburuza mkia wa kundi lake baada ya kuchabangwa katika mecjhi zote tatu za hatua ya makundi.

CHAN ni michuano inayofanana na ile ya CAN, tofauti ikiwa ni ile ya Chan kujuisha nyota wanaocheza soka katika ligi za ndani, tofauti na CAN inatyokusanya ntota kutoka popote duniani.

Uganda italazimika kuifuata Tanzania ugenini katika mechi ya kwanza itakayochezwa kati ya Juni 21 na 23, kabla ya kurudiana kati ya Julai 5 hadi 7, kupata mshindi wa kusonga mbele.

Michuano ya awali uchezwa kwa mtindo wa kanda. Timu mbili zitafuzu kuitokea Kanda ya Kaskazini, kama ilivyo kwa Kanda ya Magharibi A.

Kanda ya Magharibi B itatoa washindi watatu, watatu wengine watatokea Kanda ya Kati, huku Mashariki na Kati ikitoa watatu na mbili zitatoka Kanda ya Kusini, zitakazojumuika na wenyeji Afrika Kusini.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.