VECO KUBORESHA ZAO LA ALIZETI CHUNYA MBEYA


SHIRIKA la  VECO limesema kuwa litashirikiana na wakulima wa zao la Alizeti katika wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya  na tayari limeanzisha mpango  wa ujenzi wa  majengo yatakayotumika kwa kwa lengo la kuboresha soko  la mazao yao.

VECO limesema kuwa limetoa vifaa na gharama za ujenzi ambao una lenga kujenga majengo  katika kata za Matundasi,makongorosi,Kanga(tete),Chalangwa na Sangambi  na kuwa maeneo mengine ni Matanila na Ifumbo.


Alisema   lengo la mpango huo wa kuhimiza kilimo cha alizeti ambao upo katika hatua ya pili una lenga kuboresha maisha ya wakazi wa wilaya hiyo, ili waweze kujiongezea kipato kutokana na kuuza bidhaa  zao pamoja na kuwawezesha kuhifadhi mazao ya chakula.

Aidha Majaliwa alisema katika awamu ya kwanza iliyoanza mwaka 2004-2005 iliwezesha kuwahamasisha wakulima wa zao hilo  kutoka wakulima 200  hadi  1600 ambao ni sawa na asilimia 70,ambao  walikuwa ni wanawake  na kuwa katika awamu ya pili ya mwaka 2009 -2014 shirika hilo lina mapango wa kuhakikisha linavuka malengo yake kwa kiwango kikubwa ili  kuwaondolea wananchi hali ya umasikini.

Majaliwa alibainisha kuwa kuna idadi kubwa ya wakulima wa wilaya hiyo wanaoishi katika hali ya umasikini mkubwa, kutokana na wakulima wanache kutegemea zao la tumbaaku na kuwa hali hiyo imekuwa ikisababisha uharibifu mkubwa wa mazingira unaosababishwa na  ukataji miti ovyo.

Kwa upande wao baadhi ya wakulima wa zao hilo wamepongeza  uamuzi wa shirika la VECO kwa kuamua kuimarisha zao  hilo wilayani Chunya, kwa kuwa litawawezesha wakulima wengi kujiimarisha kiuchumi kutokana na kuishi katika hali ya umasikini kwa muda mrefu kutokana na kutegemea zaidi zao la Tumbaku  kwa muda mrefu.

Mmoja wa wakulima hao Frank Kavinga alisema tangu kuanzishwa kilimo  cha alizeti wilayani humo na kisha shirika la VECO kuanzisha mpango wa kuliendeleza zao hilo, kumekuwa na mwamko wa wakulima wengi kulima alizeti badala ya zao la Tumbaku.


Alisema  wengi wa wakulima wamekuwa wakipewa elimu ya mara kwa mara  kuhusiana na faida za kilimo cha alizeti na kuwa VECO imekuwa msitari wa mbele kuwagawia wakulima  mbegu za bure za zao hilo kwa lengo la kuharakisha kasi ya kilimo hicho.

Uamuzi wa mpango huo wa ujenzi wa majengo katika kata saba za wilaya hiyo ya Chunya unalenga kuwawezesha wakulima kukusanya na kuzalisha mazao ya alizeti kwa pamoja na kuweza kuyauza kwa faida.

Kwahisani ya Kalulunga

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.