VURUGU ZA CHADEMA ILEMELA MWANZA

 Mbunge wa Jimbo la Ilemela (CHADEMA), Highness Kiwia  (mwenye kombati ) akizungumza na waandishi wa habari , hawapo pichani kuhusu  vurugu zilizosababisha mkutano wa Kamati Tendaji ya chama hicho  kupendekeza majina ya wagombea kiti cha Meya na Naibu Meya kwenye halmshauri ya wilaya ya Ilemela

diwani wa Kata ya Kitangiri henry Matata, akizuiwa na mmoja wa wafuasi wake  baada ya kutaka kumpiga aliyekuwa Meya wa jiji la Mwanza,, Josephat Manyerere (hayupo pichani) jana kufuatia wafuasi wa diwani huyo kuvuruga mkutano a kamati tendaji ya CHADEMA wilaya ya Ilemela kushindwa kupendekeza majina ya wagombea kiti cha Meya na naibu meya.kulia ni Afisa upelelezi wa Makosa ya Jinai Wilayani humo (OC-CID) Magesa Magesa pamoja na askari wa FFU wakismzuia Matata asichue hatua hiyo.
 baadhi ya Vijana wanaosadikiwa kuwa wapiga kura na wafuasi wa diwani Henry Matata Chadema, Kitangiri wakiingia na kutoka katika ukumbi  uliokuwa na wajumbe wa mkutano a kamati tendaji ya chama hicho kujadili na kupendeza majina ya wagombea  kiti cha Meya na naibu Meya jana.Vijana hao wapato 100 waliusambaratisha mkutano huo kabla ya polisi kuwatawanya muda mfupi .

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI