WABUNGE WA SOMALIA LEO WAMEPIGA KURA KUMCHAGUA RAIS MPYA.
Bunge la nchini Somalia leo limepiga kura kumchagua rais mpya ikiwa ni hatua kuelekea katika kumaliza miongo kadhaa ya vita nchini humo.
Wabunge hao wapya wamekusanyika katika Chuo cha Polisi mjini Mogadishu kupiga kura za siri.
Miongoni mwa wagombea 25 wa nafasi hiyo ni pamoja na rais wa sasa Sharif Sheikh Ahmed na Waziri Mkuu Abdiweli Mohamed Ali.
Tayari watu wanne wameshinda na kuingia awamu pa pili ya kupigiwa kura, akiwemo Rais wa Sa na Waziri Mkuu wa sasa.
Comments