WACHIMBAJI MADINI WAREJEA MIGODINI


Wachimba migodi wa kampuni ya Lonmin nchini Afrika Kusini, wamekubali kurejea kazini siku ya Alhamisi.
Wachimba migodi hao walijawa na furaha huku wakishangilia walipoambiwa kuhusu pendekezo la asilimia 22 la nyongeza ya mishahara watakayolipw

Lakini shirika la kushughulikia mizozo ya ajira liliambia BBC kuwa lilikuwa linasubiri ikiwa pendekezo la hivi karibuni la mishahara litakubalika au la.

Mwezi jana polisi waliwaua kwa kuwapiga risasi wafanyakazi wa mgodi huo waliokuwa wakigoma kudai mishahara bora na mazingira mazuri ya kazi. Wachimba migodi 34 waliuawa.

Uzalishaji wa madini umeathirika sana kwa wiki kadhaa huku mzozo huo ukisambaa hadi katika migodi mingine.
Tume ya maridhiano iliambia BBC kwamba waakilishi wa wafanyakazi hao, waliwashauri wachimba migodi kuhusu pendekezo la sasa la nyongeza ya mishahara na wala hawakupata pingamizi zozote.

Wafanyakazi hao , walikusanyika katika uwanja mmoja karibu na mgodi wa Marikana kusikiliza hotuba ya waakilishi wao.

Wamekuwa wakidai nyongeza ya mishahara ya dola miatisa thelathini na tano. Kwa sasa wanalipwa kati ya randi 4,000 na 5,000.

''Kilichofanyika leo ni ushindi mkubwa kwa wafanyakazi hawa na watarejea kazini siku ya Alhamisi'' alinukuliwa akisema kasisi mmoja aliyewawakilisha wafanyakazi hao, Joe Seoka.

Pia alielezea kuwa wafanykazi hao watalipwa randi 2,000 kwa kipindi ambacho walikuwa wanagoma kwani hawakuwa wanapokea malipo yoyote.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI