Wageuza Tanesco kuwa shamba la Bibi.

Meneja wa Tanesco Mkoa wa Temeke Richard Mallamia, akionyesha namna umeme ulivyounganishwa kimakosa na wezi huko Toangoma.
Wahandisi wa shirika hilo wakiangalia  baadhi ya nguzo zilizo katwa na wezi hao.
 Fundi akiondoa mita ya wizi kwenye nyumba hiyo iliyokutwa imeunganishwa umeme kinyemela.
 Gari la Tanesco likibeba vipande vya nguzo vilivyokatwa katwa na wezi.
 Hapa gari la Tanesco liking'oa nguzo hizo za wizi.

 
Na Said Powa wa Raha za Pwani Blog
KATIKA haliisiyokuwa yakawaidaShirika la umemeTanzania (Tanesco) MkoawaTemeke jijini Dar es Salaam limegundua wizi wa ainayake baada ya kukamata nguzo zaidi ya 6 nanyayazake zaidi ya mita 600 zilizo sambaziwa umeme mitaani na wezi kwa kushirikiana na wenye nyumba.
 
Akizungumzia tukio hilo mbele ya waandishi wahabari wakati wa operesheni hiyo iliyofanywa kwenye eneo la Toangoma Kigamboni jijijini humo Meneja wa Mkoa wa Tanesco Temeke Mhandisi Richard Mallamia, alisema wamepenyezewa taarifa za wizi huo na raia wema natayari kabla ya kufika kwenye operesheni hiyo uchunguzi wa awali unaonyesha kuna uwezekano wa watendaji wa shirika kuhusika na tukio hilo.
Aidha kwenye zoezi hilo ambalo lilikuwa kama la kushitukiza kwenye eneo la Toangoma Masaki mmiliki wanyumba moja ambayo walikutwa mafundiwakiendelea na ujenzi aliunganisha umeme kwakushirikiana na wezi hao kwa kujichomekea nguzo zake mbili hadi kufikia nyumbayake ikiwa niumbali wa zaidiyamita 200 bila ya kufuata taratibu za shirika.
 
Akielezea tukio hilo Mhandisi wa Mkoa huo Ebenezer  Fue, alisema pamoja na kutofutwa kwa taratibu za uunganishaji kwenyeshirika lakinipia uunganishwaji wenyewe wa umeme ni wahatari kwakua haujazingatia viwango vya kitaalamu vinavyokubalika.
 
“Hizi nguzo zilizotumika hapa sizo za kusambaza umeme hukumtaani ndiomaana unaona wamezikatakata ili waweze kuzituumia na hatabaadhi ya viunganishi vya kwenye nguzo haviunganishwi kama hivi inavyoonekana,” alisema Fue.
 
“Hivi vifaa vyote ni vya shirika lakini vimefikaje huku nanani kavileta huku, ndio hatua hii tuliyoanza kuchukua sasa itatubainishia, ingawa tumeanza kutajiwa majina ya baadhi ya wahusika wa kazi hii ambao wamo ndani ya shirika lakini nimapema sana kuwataja kwasasa ngoja tuendelee na kukusanya taarifa zaidi” Mhandisi Malamia alifafanua.
 
Kwa mfumo huohuo operesheni hiyo ilibaini maeneomengine mawili kwenyekitongoji hicho cha Toangoma ambako nako pia zimechomekwa nguzo nne zikiwa na nyayazake hukuwateja hao wakisubiri hatua za mwisho kuingiziwa umeme ndani ya nyumbazao huku shirika hilo likiwa halina hata taarifa za wateja hao
Lakini jambo baya zaidi na la kusikitisha linalofanywa na wezi hao wamekuwa wakikata nyaya kwa wateja waliounganishiwa umeme kihalali kwenye mitaa na kuchukua nyaya zake kwenda kuunganishia watu wengine huku wakiwakosesha umeme watu wengine.
 
MsafarawashirikashirikahilouliongozwanaMenejawaWilayayaKigamboniInjiniaEustardEdward, ulifikahadieneoambalofamiliakadhaazimekosaumemebaadayanyayazakekuibwanakwendakuunganishiwawatuwengine.
Kwamujibu wataratibu za shirika hilo ‘service line’ za umeme zote zinakuwa tayari kwenye ramani ya shirika kwenye eneo lote la kusambaza umeme lakini wateja walikutwa na umeme huo hata kwenye shirika ramani hiyo haipo kwa hiyo mojakwamoja haoni wezi na wanpaswa kuchukuliwa hatuaza kisheria.
 
Hatahivyo Mhandisi Mallamia alisema wizi huo umelitia hasara shirika kwasababu hatanguzo zilizotumika kusambaza umemehuo sio nguzo za umemewa mtaaani ni nguzo kubwa za kusambaza umeme kwenye laini kubwa, na ndiomaana wamelazimika kuzikata zaidi ya maramoja ili ziweze kuendana sawa ambapo alisema kufanya hivyo nihasara kubwa kwani nguzo moja pekee thamani yake karibu Tsh2Millioni.
 
Aidha Mallamia amewapongeza watanzania wenye uchungu na shirikalao kwakutoa taarifa za wizi huo na kuwataka kufanya hivyo mara kwa mara ili kufichua uovu huo.
 
Tangu Shirika hilo kufungua ofisi za kanda Mikoa na Wilaya na kuwa na Mameneja wenye meno kumekua na ufanisi kiutendaji ndani ya shirika kwa kuweza kufuatilia matukio kwa haraka.
MWISHO:

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.