WANAHABARI MWANZA WALIVYOANDAMANA KULAANI MAUAJI YA MWANGOSI

 Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mwanza (MPC) Deus Bugaywa akisoma barua ya zuio la polisi kufanyika kwa maandamao hayo ya wanahabari kwa jiji la Mwanza ili kupisha ziara ya Waziri Mkuu sababu ambazo hazikuafikiwa na waandishi wote nao wakaendelea na zoezi la kuandamana kutoka viwanja vya Ghand hall jijini Mwanza  kupitia barabara kadhaa hadi uwanja wa Nyamagana jijini hapa.
 Twalad Salum wa gazeti la Mzawa, akiwa amebeba bango lenye ujumbe kamwe kalamu haiwezi kunyamazishwa kwa risasi.Chama cha Waandishi wa Habari mkoa wa Mwanza (MPC) kimepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha kinyama cha mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha channel ten, mkoani Iringa, Daudi Mwangosi akiwa mikononi mwa jeshi la polisi mkoa wa Iringa.
 Jane Kajoki akiwa amebeba bango lenye picha ya marehemu Daudi Mwangosi likiwa na ujumbe usemao Mwangosi umekufa ukilitumikia taifa.Nyuma ya kajoki ni Deus Buganywa mwenyekiti wa MPC.Marehemu Mwangosi alikuwa Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC), aliuawa akiwa kazini september 2,2012 katika moikono ya polisi waliokuwa katika kazi maalum huko Nyololo, Iringa.
 Maria Philbert akiwa na bango lenye ujumbe baada ya Mwangosi nani atafuta?"Mauaji ya Mwangosi yamebadili sura ya Tanzania kimataifa kuwa ni kisiwa cha amani na sasa kuwa ni kisiwa cha mauaji, kwani Mwangosi amekuwa ni mwanahabari wa 38 kufa akiwa kazini kuanzia mwezi Januari 2012 hadi september 2012 Duniani, na haya ni mauaji ya kwanza kwa mwandishi kufa akiwa kazini.


 Waandishi wa habari Mwanza, wakiomba dua baada ya kuhitimisha maandamano kupinga mauaji ya Mwangosi,kwenye uwanja wa Nyamagana jijini
Kwa nini askari polisi wamegeuka kuwa wauaji?Nani amewatuma polisi kufanya mauaji?Kwa nini wanafanya hivyo hawachukuliwi hatua?Ni nani anayewafanya polisi wawe juu ya sheria?Taarifa za awali zinaonyesha kuwa Mwangosi kabla ya kufikwa na mauti katika kijiji cha Nyololo, Mufindi alizingirwa na kushambuliwa na polisi waliokuwa katika eneo la tukio na hata alipopiga kelele za kuomba msaada, hakusikilizwa na matokeo yake aliuawa kikatili. pix 6 wakiwa katika picha ya pam,oja baada y maandamano


Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.