Waziri Muhongo, Atangaza Kiyama Kwa Atakaye Saini Mikataba Mibovu

                   Profesa sospeter Muhongo.

Na:  Datus Boniface

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amewaonya maofisa wa Wizara pamoja na wa taasisi zingine zilizopo chini ya Wizara yake kuwa, atakayeliingiza taifa kwenye Mikataba mibovu atafukuzwa kazi na kushtakiwa.Pia amesema Ofisa anaweza kufukuzwa au kusimamishwa kazi endapo ikibainika kuwa Mkataba aliyousaini una harufu au fununu za rushwa.
Aidha, amewaonya Wakurugenzi wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC), kuwa hatakuwa tayari kusaini mikataba yoyote, kabla wao kuipitia na kuridhishwa nayo.Waziri alikuwa akizungumza hayo jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi wa TPDC.
“Moja ya kazi zenu ni kupitia kila Mkataba na kuona kama una manufaa, lakini pia hakuna Mkataba mpya nitasaini bila Bodi kuupitia” alisema. Alisema uzoefu unaonyesha kuwa pesa nyingi za serikali hupotea kutokana na mikataba mibovu iliyosainiwa.
Bodi hiyo mpya ina wakurugenzi 10 ikiongozwa na Michael Mwinda ambaye ni Mwenyekiti, Robert Kahyoza, na Mwalim Ali Mwalim na wengine.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA