WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YATOA UFAFANUZI JUU YA BARABARA YA SERENGETI


Wizara ya Maliasili na Utalii imefafanua kuwa barabara ambayo nchi ya Ujerumani imependekeza kuwa ingependa kuifadhili ni ile ambayo inaanzia Mto wa Mbu mkoani Arusha kwenda Mkoani Mara kwa kupitia nje ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti upande wa Kusini. Barabara iliyopendekezwa haitapita kabisa ndani ya Hifadhi hiyo.
Ufafanuzi huu umetolewa baada ya magazeti mawili ya hapa nchini yanayotolewa kwa lugha ya Kiingereza (toleo la tarehe 4 Septemba) kuandika kuhusiana na barabara hiyo bila kuweka wazi kuhusu ramani ya barabara ambayo Naibu Balozi wa Ujerumani aliitaja hivi karibuni alipomtembelea Waziri wa Maliasili na Utalii
Aidha, gazeti mojawapo kati ya hayo mawili, toleo la tarehe 5 Septemba 2012 liliandika tahariri iliyoonyesha kuwa barabara iliyopendekezwa itapita ndani ya Hifadhi ya Serengeti upande wa Kaskazini, hiyo siyo kweli maana Naibu Balozi hakusema hivyo.
Mazungumzo kuhusu suala hili la barabara ya Serengeti yalifanyika tarehe tarehe 3 Agosti 2012 wakati Naibu Balozi wa Ujerumani wa hapa nchini Bw. Hans Koeppel alipomtembelea Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe Khamis Kagasheki na kumwambia kuwa nchi yake iko tayari kufadhili upembuzi yakinifu na ujenzi wa barabara itakayozunguka Hifadhi ya Taifa ya Serengeti upande wa Kusini kama nchi hiyo itaombwa kufanya hivyo. Waziri Kagasheki alilipokea pendekezo hilo na kuahidi kulipeleka kwa Waziri wa Ujenzi Mhe Dkt Magufuli.
[MWISHO]
George Matiko
MSEMAJI
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.