YANGA YATIMUA VIONGOZI WOTE WA KUAJIRIWA, WAMO SENDEU NA MWESIGWA

Sanga akizungumza na Waandishi wa Habari mida hi. kulia ni Tito Osoro, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji na kushoto Isaac Chanji, Mjumbe wa kuteuliwa


Mkutano na Waandishi
Na Mahmoud Zubeiry
UONGOZI wa klabu ya Yanga ya Dar es Salaam, umeisimamisha kazi Sekretarieti nzima ya klabu, akiwemo Katibu Celestine Mwesigwa na Ofisa Habari, Louis Sendeu, kutokana na kile ilichoeleza utendaji usioridhisha.
Akizungumza na Waandishi wa Habari ‘mida hii’ makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga alisema kwamba maamuzi hayo yamefuatia kikao cha Kamati ya Utendaji kilichofanyika tangu saa 5:30 leo hadi saa 9:30.
Wengine wanaokumbwa na panga hilo ni Masoud Saad, aliyekuwa Ofisa Utawala, Philip Chifuka aliyekuwa Mhasibu na Hafidh Saleh aliyekuwa Meneja ambaye anahamishiwa kwenye majukumu mengine.
“Tumesitisha mikataba ya sekretarieti nzima, pia tumefanya marekebisho, tumemtoa Meneja wa timu na muda si mrefu tutamtangaza Meneja mwingie pamoja na sekretarieti mpya,”alisema Sanga.
Aidha, Sanga alisema Kocha Mbelgiji, Tom Saintfieti anapewa onyo kali kwa kuzungumza ovyo na vyombo vya habari.
“Tumekwishakutana naye mara kadhaa kumpa utaratibu wa kuzungumza na vyombo vya habari, sasa tutamuandikia barua ya kumkumbusha wajibu wake na kuzingatia wajibu wake, kutozungumza na vyombo vya habari holela,”alisema.
Kwa ujumla maamuzi haya yanakuja baada ya Yanga kuanza vibaya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ikiambulia pointi moja tu katika mechi zake mbili za awali, kutokana na sare ya bila kufungana na Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya Jumamosi na Jumatano ikachapwa mabao 3-0 Morogoro Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA