YANGA,SIMBA WAKABIDHIWA MAGARI NA TBL


 Wapenzi wa Simba wakitumbuiza huku wakiwatania watani wao wa jadi Yanga kwa kipigo cha mabao matatu kwa nunge dhidi ya Mtibwa Suger, jana wakati wa hafla ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kuzikabidhi Yanga na Simba mabasi mapya makubwa mawili yenye thamani ya sh. mil. 450, Dar es Salaam leo.

 Wapenzi wa Yanga wakiwatania watani wao wa Simba kwa kuwazidi kete kuwa kumchukua Mbuyu Twite
 Yanga wakitumbuiza wakati wa hafla hiyo
 Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, Robin akibadishana hati na Mwenyekiti wa Simba, Aden Rage
 Mkurugenzi Mtendai wa TBL, Robin akibadailishana hati na Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga
 Gari jipya la Yanga
 Gari jipya la Simba
 Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, Robin akimkabidhi mfano wa ufunguo wa basi, Mwenyekiti wa Simba, Aden Rage
 Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, Robin akimkabidhi mfano wa ufunguo wa basi, Mwenyekiti wa Yanga, Cement Sanga
 Viongozi wa TBL na Yanga na Simba wakiwa katika picha ya pamoja
Mkuu wa Usambazaji na Mauzo wa TBL, James Bokella akipepea bendera  ikiwa ni ishara ya kuyaruhusu mabasi hayo kuondoka katika Makao Makuu ya TBL leo


Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia yake ya Kilimanjaro Premium Lager leo imetoa mabasi mawili kwa klabu za Simba na Yanga. Mabasi hayo ya kifahari yana thamani zaidi ya Sh milioni 450.

Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika Makao Makuu ya TBL, mbele ya Mkurugenzi Mkuu wa TBL, Robin Goetzsche pamoja na makundi ya Simba na Yanga pamoja, wadau mbalimbali wa mpira wakiwemo pia waandishi wa habari. Kununuliwa kwa mabasi hayo kumefanywa na TBL kwa mujibu wa mkataba baina yake na klabu hizo kubwa nchini.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu alisema: “Tunaona heshima kubwa sana kuwa na uhusiano na klabu hizi ambazo daima zina mafanikio.

 “Malengo yetu ni kukuza soka nchini Tanzania na kwa kuanzia tumeona tushirikiane na Simba na Yanga ambazo kila zinapokutana uwanjani hali huwa ya kuchangamka sana katika mwendelezo wa Ligi Kuu.”
Alisema mabasi hayo yaliyotolewa kwa klabu hizo, yalenge kuinua soka na kuzitaka klabu hizo kuyatunza mabasi hayo kwa maslahi ya wachezaji na watendaji wengine. “Tutaendelea kuwapa msaada pale kwa vile tunatarajia kuwa mtaleta faida kwa maana ya matokeo mazuri katika soka kwa kutwaa mataji na kama wengi tujuavyo, mpira ni mabao.”

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe alisema mabasi hayo yenye uwezo wa kubeba watu 51 yamenunuliwa kutoka Yutong.

Alisema mabasi hayo ni ya kisasa kabisa kwani yanabeba abiria 51 akiwemo dereva, ni imara kwani chasis yake ni 4x2, injini ya mabasi haya ni aina ya  300 HP Cummins, yana  retarder ya umeme and breki aina ya ABS, yana TV mbili za kisasa, muziki wa nguvu wenye spika nane, milango na mabuti ya kisasa, kioo cha kuangalia nyuma kinachotumia umeme, jokofu na  kiyoyozi.

“Tunataka wachezaji wetu wawe na raha wanaposafiri. Hii ndiyo maana tumeamua kutoa mabasi haya ya kifahari ambayo ndani yake kuna huduma muhimu kama televisheni, friji, vitu ambavyo tunaamini mtavitunza.”
Aliongeza kuwa pamoja na ukweli kwamba TBL inawajibika kununua mabasi hayo kwa mujibu wa mkataba, lakini lengo kuu ni kuona kuwa wachezaji wanakuwa katika mazingira mazuri.

Baada ya makabidhiano hayo, wahudhuriaji kutoka klabu hizo walicheza na kufurahia mabasi hayo huku wakiimba nyimbo mbalimbali.

Bia ya Kilimanjaro ilianza kuzidhamini Simba na Yanga tangu mwaka 2008.

Kuhusu TBL
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), ni watengenezaji na wauzaji wa bia safi pamoja na vinywaji mbalimbali visivyo na kileo. TBL ina hisa katika Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited na Kampuni Mama ya Mountainside Farms Limited.

Baadhi ya vinywaji ni pamoja na Balimi Extra, Eagle, Eagle dark, Bia Bingwa, Maji ya Safari, Ndovu Special Malt, Castle Lite, Kilimanjaror, Castle, Castle Milk Stout, Redd’s Original, Grand malt, Miller Ginuine Draft, Peroni. Vingine ni Konyagi Gin na Amarula Cream.

TBL imo katika orodha ya Soko la Hisa la Dar es Salaam huku ikiwa na wafanyakazi wapatao 1,300. Ina mawakala na wasambazaji kote nchini na viwanda vitatu makini.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*