BAADA YA KUFUNGWA NA MTIBWA SUGAR, MASHABIKI WA SIMBA WAKUSANYIKA MAKAO MAKUU YA KLABU YAO WAKIWA NA MABANGO


 Mashabiki wa timu ya Simba wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali, Makao Makuu ya klabu hiyo Mtaa wa Msimbazi jijini Dar es Salaam jana, kuonesha hasira zao baada ya timu hiyo kusuasua katika michezo yake ya Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara, ambayo ilifungwa bao 2-0 na Mtibwa Sugar, kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. (Picha na Habari Mseto Blog)
 Ujumbe kwa golikipa wa Simba, Juma Kaseja
Mashabiki wa timu ya Simba wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali, Makao Makuu ya klabu hiyo Mtaa wa Msimbazi jijini Dar es Salaam jana, kuonesha hasira zao baada ya timu hiyo kusuasua katika michezo yake ya Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara, ambayo ilifungwa bao 2-0 na Mtibwa Sugar, kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro juzi. (Picha na Habari Mseto Blog)


BAADA ya kupata kipigo cha mabao 2-0 wapenzi wa klabu ya Simba, leo walifurika katika makao makuu ya klabu hiyo wakiutaka uongozi wa klabu hiyo ujiuzulu.

Mashabiki hao walionekana wakiimba nyimbo mbalimbali wakiwataka viongozi wa klabu hiyo kujiuzulu, kwa kuwa wanaonekana hawapo makini na timu yao.

Jambo Leo ilishuhudia mashabiki hao wakitoa maneno makali dhidi ya viongozi wao ambao hawakuwepo katika klabu hiyo katika siku hiyo ya leo.

"Tunaomba waondoke wenyewe tayari timu imeshawashinda maana tulikuwa tunatoka sare jana tumefungwa kabisa na Mtibwa Sugar...waondoke watuachie timu hiyo"alisema Salim Ramadhan.

Hata hivyo kipigo hicho pamoja na kutoka sare mfululizo kwa timu ya Simba, wadau wa soka wamemtaka kipa namba moja wa timu hiyo Juma Kaseja kupumzika.

Kaseja ambaye amedaka toka michuano ya kombe la Kagame pamoja na ligi kuu inayoendelea mpaka sasa hajapumzika hali inayoshukiwa huenda matokeo mabaya pia yanachangiwa na kipa huyo kuchoka.

Wakizungumza na Jambo Leo wadau hao wamesema Simba ni timu nzuri na yenye wachezaji wenye viwango vizuri lakini mwalimu anapaswa kuwatumia wachezaji wengine ambao wanaonekana wana viwango lakini muda mwingi hukaa benchi.

"Ifike wakati Kaseja naye apumzishwe,sio nasema hivi kwa maana ya kumpangia kocha timu lakini kila mdau wa soka analiona hili huwezi kumchezesha mchezaji kw a muda mrefu hivyo,hata yeye anahitaji kupumzika na kupata muda wa kujipanga upya hivyo mwalimu aliangalie hili kwa umakini"alisema Kennedy Mwaisabula.

Mwaisabula aliongeza kuwa Kikosi cha Simba kina kazi kubwa ya kurudisha imani ya mashabiki wao na pia kina michuano mikubwa ya kimataifa mbele yao hivyo maandalizi yao kuanzia sasa ndio yatakayowasaidia kufanya vizuri katika michuano ya klabu bingwa Afrika.

Kwa upande wa mchezaji wa zamani wa timu hiyo Zamoyoni Mogella aliunga mkono juu ya kupumzishwa kwa kipa huyo huku akitaka uongozi wa timu hiyo kutulia kwa sasa na kuangalia mapungufu ya wachezaji wao.

"Wapo makipa wazuri kama Albert Mweta,Hashim ambao wanaweza kudaka ukiachilia Kaseja ambaye mara nyingi amekua akichezeshwa,ni vyema akapewa muda apumzike kidogo na wengine wapewe nafasi"alisema Mogella.

Naye Joseph Kanakmfumu ambae ni kocha na mdau wa soka amesisitiza Simba inatakiwa kuhakikisha inajipanga vyema kuelekea mashindano ya kimataifa kwani ipo katika mwenendo wa kusuasua na inahitaji umakini zaidi katika kujipanga vyema.

Simba imebakiza mchezo mmoja kabla ya kuhitimishwa kwa duru ya kwanza ya ligi kuu Tanzania bara ambapo itavaana na Toto Afrikan ya Mwanza kwenye uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA