BREAKIING NEWSSSS BASI LA ABOOD LAPINDUKA MBEYA

BASI la kampuni ya Abood inayofanya safari za Mbeya na Dar Es Salaam juzi ilipata ajali na kusababisha kifo cha kondakta wake na kujeruhi abiria zaidi ya 23 baada ya kugongana uso kwa uso na Roli.
Ajali hiyo ilitokea katika eneo la Sae Jijini Mbeya majira ya saa 12:45 jioni wakati basi hilo likitokea Dar Es Salaam na kuelekea Kituo kikuu cha Mabasi Mkoani hapa.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athmani alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo alimtaja marehemu wa basi hilo kuwa ni Charles Kiteleke(42) mkazi wa Morogoro ambaye alikuwa ni Kondakta.
Alisema Marehemu alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa kufuatia majeraha aliyoyapata kwenye ajali hiyo.
Katika ajali hiyo abiria 23 walijeruhiwa kati yao 15 walipatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mbeya na kuruhusiwa huku watu 8 wakiendelea kupatiwa matibabu Hospitalini hapo.
Alizitaja namba za Basi hilo kuwa ni T545 AZE Scania mali ya Kampuni ya Abood likiwa linaendeshwa na dereva Mussa Kilasi Mkazi wa Dar es Salaam ambapo Lori lililogongana nao lilikuwa na namba za usajili T610 ATQ/T253 APL Scania.
Aliwataja majeruhi waliolazwa kuwa ni Nicus Kayuni, Mfany, Andrea Mbila , Zamoyoni Watson, Vumilia Mwazembe Alinamaka Mahenge, Anka Myambo, Hilda Chilwa na Gift Nankali wote wakazi wa Tunduma wilayani Momba.
Diwani, alisema chanzo cha ajali hiyo kimetokana na mwendokasi wa gari T 610 ATQ likiwa na Tela lenye namba za usajili T253 APL scania ambalo lilikuwa linajaribu kupita gari lingine hivyo kwenda kugongana na basi hilo.
Hata hivyo Kamanda Diwani alisema Jeshi la polisi mkoani Mbeya inaendelea kuwatafuta madereva wa magari yote mawili kwani mara baada ya tukio walikimbia na kwamaba amewataka madereva kuzingatia sheria sheria za usalama barabarani.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*