BRIGITTE ALFRED NDIE REDDS MISS TANZANIA 2012
HATIMAYE kile kitendawili
cha muda mrefu cha Nani ata twaa taji la Redds Miss Tanzania 2012, kimeteguliwa
usiku wa Novemba 3, 2012, baada ya Mrembo kutoka Kitongoji cha Sinza na Kanda ya
Kinondoni jijini Dar es Salaam, Brigitte Alfred kutwaa taji
hilo.
Brigitte ambaye nyota yake
katika mashindano hayo ya urembo nchini ilianza kung’aa tangu Kitongoji cha
Sinza baada ya kutwaa taji la Sinza na Baade kutwaa Taji la Redds Miss Kinondoni
amedhihirisha ukali wake baada ya kuwabwaga warembo wenzake 29 waliokuwa
wakiwania taji hilo kutoka Kanda mbambali.
Mpinzani mkubwa wa Brigitte
katika shindano hilo alikuwa ni Mrembo kutoka Kanda ya Ziwa ambaye nae alianza
kuwika baada ya kutwaa taji la Redds Mkoa wa Mara na baade kutwaa taji la Kanda
ya Ziwa, Eugene Fabian.
Enagene alifanikiwa kushika
nafasi ya pili katika shindano hilo kubwa ambalo Brigitte ameondoka akiendesha
gari aina ya NOAH na kitita cha Shilingi Milioni 8.
Nafasi ya tatu ilikwende
kwa Malkia wa Kitongoji cha Kigamboni City na Miss Temeke 2012, Edda Sylvesta
huku nafasi ya Nne ikichukuliwa na Mrembo wa Dar Indian Ocean na Kinondoni,
Magdalena Roy na nafasi ya Tano ikienda Kanda ya Ziwa tena kwa Mkoa wa Mwanza,
Happyness Daniel.
Brigitte Alfred akipunga
mkono kwa furaha mara baada ya kutangazwa kuwa ndie mshindi na kuwabwaga
washiriki wenzake 29.
Brigitte Alfred (kulia)
akiwa katika picha ya pamoja na Miss Tanzania 2011, Salha Izrael
Mshindi wa Taji la Redds
Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred (katikati) akipunga mkono kwa furaha katika
picha ya pamoja na mshindi wa Pili, Eugene Fabian (kushoto) na Mshindi wa Tatu,
Edda Sylvester mara baada ya warembo hao kutangazwa kuwa washindi wa shindano
hilo. Brigitte anatokea Kitongoji cha Sinza na Kanda ya Kinondoni wakati, Eugene
anatoka Mkoa wa Mara na Kanda ya Ziwa huku Edda ni Miss Kigamboni na Kanda ya
Temeke.
Warembo waliofanikiwa kuingia hatu5 bora ya Redds Miss
Tanzania 2012, kutoka kushoto ni Brigitte Alfred, Eugen Fabian, Happyness
Daniel, Edda Sylvester na Magdalene Roy wakipozi kwa picha.
Washiriki wakicheza show ya ufunguzi wakati wa
kuanza kwa shindano hilo.
Wageni mbalimbali na wadau wa tasnia ya Urembo
nchini Tanzania wakifuatilia shindano hilo kwa umakini ndani ya Ukumbi wa Ubungo
Plaza jijini Dar es Salaam.
Wasanii wa kundi la Ngoma za Asili la Wanne Stars
likitoa burudani kwa wageni.
Balozi wa Tanga Beach Resort, Happyness Rweyemamu
akijinadi jukwaani na vazi lake la ubunifu.
Mshiriki Flavian Maeda kutoka Kitongoji cha Kurasini
na Kanda ya Temeke jijini Dar es Salaam akipozi jukwaani na vazi la
ubunifu.
Fina Recatus akipita jukwaani na vazi la ubunifu.
Fina ni Balozi wa Tanga Beach Resort 2012.
Naomi Jones nae akipita jukwaani na vazi la
ubunifu
Mrembo wa Dar Indian Ocean na Kinondoni, Kudra
Lupato nae alikatiza jukwaani na kunaswa na Camera ya Father Kidevu
Blog.
Brigitte
akipozi na vazi lake la Ubunifu
Msanii kutoka
THT Rachel nae alipata fursa ya kuonesha kipaji chake na kudhihirisha wazi kuwa
yeye ni Mrithi wa Ray C kwa sauti na kiuno Bila mfupa.
Japokuwa ni ufukweni lakini chini walivaa hivi, maana
shindano la Dunia ndivyo inavyokuwa
Warembo
mbalimbali wa Redd's Miss Tanzania 2012 wakionekana Jukwaani katika vazi la
ufukweni.
Warembo
mbalimbali wa Redd's Miss Tanzania 2012 wakionekana Jukwaani katika vazi la
ufukweni.
Warembo
mbalimbali wa Redd's Miss Tanzania 2012 wakionekana Jukwaani katika vazi la
ufukweni.
Warembo
mbalimbali wa Redd's Miss Tanzania 2012 wakionekana Jukwaani katika vazi la
ufukweni.
Mdau Kabula nae hakukosa na
haopa akiwajuza waliobaki nyumbani kinachojiri. Siunajua tena mambo ya Tanesco
baadhi ya mitaa na mikoa ilikuwa giza tu.
Juma Pinto
kutoka Jambo Concerpt (kulia) na William Malecela 'Lemutuz' nao
walikuwepo.
Waongoza Show
nzima ya Redds Miss Tanzania 2012, Jocate Mwegelo 'Kidot' na Taji Liundi
wakiwajibika.PICHA NA FATHER
Comments