''CHUCK NORRIS'APANDISHWA MAHAKAMANI IRINGA ADAIWA KUHUSIKA KUMJERUHI PAROKO WA RC ISIMANI

Watuhumiwa wa ujambazi ambao  walimshambulia paroko kwa risasi wakiongozwa na kiongozi  wao Chuck Norris katikati mbele wakipelekwa mahabusu baada ya kusomewa makosa 6 likiwemo la kujeruhi paroko na msaidizi  wake . Kwa Hisani ya Francis Godwin Blog
Watuhumiwa  wakipelekwa mahabusu

Leo  polisi walikuwa hana shida na waandishi hata pale ilipoonekana hujawapata vema watuhumiwa  walikuwa  wakiwaweka  sawa  ili upate picha nzuri tofauti ya mtuhumiwa wa mauwaji ya mwanahabari Daudi Mwangosi


Watu  saba  wakazi wa Isimani wilaya ya Iringa  mkoani Iringa  wakiongozwa na mtuhumiwa  Alex Mgunda maarufu kwa jina la Chuck Norris   wamefikishwa  mbele ya hakimu  mkazi mwandamizi mfawidhi wa mkoa  wa Iringa  Juma S.K Hassan na kusomewa makosa 6 likiwemo la   kumjeruhi kwa risasi  paroko wa Kanisa Katoliki (RC) Isimani wilayani  Iringa , Angelo Burgeo (60) na msaidizi wake, Herman Myalla (36) kabla ya kumpora fedha kiasi cha Tsh. milioni 2.5 na Euro 1000

Watu  saba  wakazi wa Isimani wilaya ya Iringa  mkoani Iringa  wakiongozwa na mtuhumiwa  Alex Mgunda maarufu kwa jina la Chuck Norris  leo  wamefikishwa  mbele ya hakimu  mkazi mwandamizi mfawidhi wa mkoa  wa Iringa  Juma S.K Hassan na kusomewa makosa 6 likiwemo la   kumjeruhi kwa risasi  paroko wa Kanisa Katoliki (RC) Isimani wilayani  Iringa , Angelo Burgeo ( 60) na msaidizi wake, Herman Myalla (36) kabla ya kumpora fedha kiasi cha Tsh. milioni 2.5 na Euro 1000

Wakili wa Serikali aliwataja watuhumia hao kuwa  Joseph Ngwale ( 30 ) ,Alex Mgunda  ( 30 ),Joshua  Mlagala ( 28 ) wote wakazi wa Isimani, Bruno Mdemu ( 47 ) ambaye ni dereva wa kanisa hilo ,Daud Ngwale ( 24 ),Elasto Ngwale ( 38 ) wakazi wa Isimani na Gaitani Kitwange ( 62 )mkazi wa Mkungugu Iringa
 
Akiwasomea  shitaka la kwanza  mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi wa mkoa Juma Hassan, la kula njama ya kutenda kosa  , Wakili wa serikali Riziki Matitu alidai kuwa  Novemba 15 mwaka huu wote kwa pamoja huko katika kijiji cha Luanja Tarafa ya Isimani Iringa Vijijini walitenda makosa hayo,ambapo washitakiwa walikana kosa hilo.
 Shitaka la  pili lilikuwa la kuvunja nyumba,Wakili Matitu alidai kuwa mnamo Novemba 15  katika kijiji cha Luanja kwenye kanisa la Katoliki la Isimani walivunja na kufanya wizi wa kutumia silaha na kujeruhi.
Wakisomewa kosa la tatu la unyang’anyi wa kutumia silaha na kuiba sh.milioni 2.8 na Euro 100, Wakili hiyo wa serikali alidai kuwa  kabla ya kutenda kosa hilo walimtishia Paroko Angelo Burgeo  Kwa silaha na kuchukua fedha hizo,huku kosa la nne na la tano  lilikuwa la kujeruhi, ambapo wote k wa pamoja pasipo uhalali  walimjeruhi  Paroko Angelo Burgeo  na Herman Myalla ambaye ni msaidizi wa Paroko huyo .
Aidha Wakili huyo akisoma shitaka la mwisho ambalo lilikuwa likimkabili Mshitakiwa wa Kwanza Joseph Ngwale kwa kutuhumiwa kumiliki silaha pasipo kihalali,Matitu alidai mahakamani hapo kuwa mshitakiwa huyo alikutwa nyumani kwake akimiliki silaha bila kibali na hivyo kuchukuliwa hatua za kisheria.

 Kwa  upande wake mtuhumiwa namba mbili  Mgunda aliiomba mahakama hiyo kumwondoa katika  kesi hiyo kwa madai kuwa yeye si makazi wa Isimani kama alivyoshtakiwa bali ni mwenyeji wa Isakalilo mjini Iringa na alikamatwa usiku akiwa nyumbani kwake .

Huku mshitakiwa namba moja katika kesi hiyo akidai kuwa maelezo aliyotoa alikuwa hajitambui baada ya kupigwa sana na polisi baada ya kukamatwa ,maombi yaliyotupiliwa mbali na mahakama hiyo kwa madai  kuwa kukamatwa Isakalilo hakuwezi kukutoa katika kesi ya msingi kwani yawezekana mtuhumiwa akatoka Zanzibar na kuja kuiba Iringa na kukamatiwa huku hivyo kuwataka wasubiri kujitetea kesi hiyo itakapoanzwa kusikilizwa.
  
Kesi hiyo ambayo ililetwa tena mahakamani hapo Desemba 6 mwaka huu ,na washitakiwa wamerudi rumande,ambapo katika kesi hiyi kisheria haina dhamana .

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.