DAVID MOSHA AREJESHWA KAMATI YA MASHINDANO YANGA

UONGOZI wa Klabu ya Yanga umewateuwa Davis Mosha, Muzamili Katunzi na Beda Tindwa katika kamati ya Mashindano huku Baraka Kizunguti akiwa Ofisa Habari na Shaban Katwila akiwa Meneja wa timu hiyo.

Akizungumza Dar es Salaam leo, Katibu Mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako, alisema kuwa maamuzi hayo yametolewa katika kikao cha kamati ya utendaji ya klabu hiyo.

Alisema waliouteliwa wataanza kazi zao mara moja katika klabu hiyo, ikiwa ni pamoja na kujulishwa uteuzi huo.

Mwalusako alisema licha ya kuwepo kwa maamuzi hayo Kamati hiyo imepanga tarehe ya Mkutano Mkuu wa wanachama ambao utafanyika Desemba 16 mwaka huu.

Alisema Mkutano  huo utafanyika kama kanuni za klabu hiyo zinavyosema ambapo kila mwaka ni lazima ufanyike mkutano wa wanachama kujua maendelea na klabu yao.

"Hayo ndiyo maamuzi ya Kikao cha Kamati ya Utendaji....ambapo kina Mosha watakuwa chini ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo Abdallah Bin Kleb na Mkutano Mkuu utafanyika Disemba 16"alisema Mwalusako.

Wakati huo huo, Kocha Mkuu wa klabu hiyo Ernie Brandts, ameipongeza timu yake kwa kuweza kupata ushindi katika mchezo wao wa juzi ikiwa ni pamoja na kufikia malengo yake.

Akizungumza mara baada ya mchezo wao dhidi ya Azam, kocha huyo alisema amefurahishwa na uwezo wakliionesha wachezaji wake katika mchezo huo ikiwa ni pamoja na kupata mabao 2-0.

Brandts alisema kwa kiwango alichokiona jana ni wazi wachezaji wake wamejipanga kuifikisha mbali timu yake ikiwa ni pamoja na kufikia malengo alijiwekea.


"Nimefurahishwa sana na uwezo wa leo ikiwa ni pamoja na kupata ushindi mnono kwa timu ngumu kama Azam ambayo hucheza mchezo mzuri kila mara"alisema Brandts.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.