DJ Too Short” ameibuka mshindi katika shindano la Hannessy DJ Challenge

Balozi wa kinywaji cha Hennessy Cyrille Auriol na Mwenyekiti wa Makampuni ya Qweensway Group, Amin Hirjee, wakimzawadia DJ maarufu nchini, DJ Too Short mkanda wa ushindi katika shindano la Hennessy DJ Challenge lililofanyika hivi karibuni kwenye ukumbi wa Serena Hotel.
Picha: Mpiga Picha wetu
………………………………..
Mwandishi Wetu
DJ Mohamed Ali  maarufu kwa jina la “DJ Too Short”  ameibuka mshindi katika shindano la Hannessy DJ Challenge lililofanyika kwenye ukumbi wa hotel ya Serena jijini.
Ushindi wa DJ Too short umetokana na jinsi alivyoweza kuwachezesha mashabiki kibao wa kinywaji cha Hennessy katika usiku maalum kinywaji hicho.
Balozi wa dunia wa Hennessy, Cyrille Auriol na  Mwenyekiti wa makampuni ya Qweensway Group, Amin Hirjee walimzawadia zawadi ya ushindi DJ huyo.
Kutokana na ushindi huo, DJ Too Short anakuwa Mtanzania wa kwanza kushinda nafasi hiyo na kuzawadiwa mkanda wa utambulisho wake na yeye kushukuru kwa mafanikio hayo.
Mbali ya tukio hilo, Balozi Auriol alikutana na wadau mbali mbali wakiwemo wafanyabiashara na wadau wa masuala ya maonyesho ya mavazi (modal) au walimbwende na kujadili changamoto mbali mbali zinazowakabili hasa wafanyabiashara wa vinywaji.
Balozi huyo alifanya ziara yake ya siku mbili, ikiwa ni miongoni mwa ziara yake ya siku tano katika nchi za Afrika Mashariki. Hii ni mara ya pili kutembelea Tanzania.
Alisema kuwa biashara ya vinywaji ambayo inawahusu wafanyabiashara, wanamuziki na sekta nyingine kwa sasa inakuwa kwa kasi pamoja na kuwepo kwa changamoto mbali mbali.
Alisema kuwa wanajitahidi kuondoa changamoto hizo na nyingi zinatokana na ushindani katika soko husika na moja ya mikakati yao ni kuwafundisha watoa huduma hiyo ili kuweza kufikia kiwango cha kimataifa. KWA HISANI YA FULLSHANGWE BLOG

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*