HAYATOU KUFUNGUA TUSKER CHALLENGE WIKI IJAYO

Hayatou kushoto akiwa na Rais wa FIFA, Sepp Blatter kulia

KWA HISANI YA BONGO STAZ BLOG
RAIS wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Issa Hayatou amekubali kuhudhuria sherehe za ufunguzi wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, Cecafa-Tusker Challenge wiki ijayo mjini Kampala, Uganda.
 
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Uganda (FUFA), Rogers Mulindwa ameiambia BIN ZUBEIRY leo kutoka Uganda kwamba, Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) tayari limepokea uthibitisho wa Hayatou kufungua michuano hiyo kutoka makao makuu ya CAF, Cairo, Misri. 
 
Bosi huyo wa soka barani, anatarajiwa kuwasili Kampala Novemba 22, kufuatia mwaliko huo wa Rais wa CECAFA, Leodegar Tenga.
 
Rais wa FUFA, Lawrence Mulindwa amesema Uganda imefurahia heshima hiyo ya ujio wa Hayatou, ambaye atafuatana na viongozi mbalimbali wa CAF, akiwemo Katibu Mkuu, Hicham El Amrani, Mohamed Raouraoua,
 
 Constant Omari na Ngangue Appolinaire. Katika ziara yake hito, Hayatou atahudhuria Mkutano wa CECAFA katiuka hoteli ya Serena Ijumaa ya Novemba 23 kabla ya kufungua rasmi michuano ya mwaka huu ya Cecafa-Tusker Cup Uwanja wa Namboole jioni ya siku inayofuata. 
 
Uganda itawakaribisha jirani zao Kenya katika mchezo wa ufunguzi wa michuano hiyo saa 10:00 jioni, Jumamosi ya Novemba 24.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

GSM ARIDHIA UJENZI WA UWANJA WA YANGA JANGWANI

WACHEZAJI YANGA WAGOMA KABISA KUFANYA MAZOEZI LEO, LWANDAMINA AIBUKA PEKE YAKE SHAMBA LA BIBI

DKT. MAJULE AMFANYIA MAPOKEZI MAKUBWA BALOZI WA CHINA NCHINI

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

Wasifu wa Kizza Besigye

HERSI KWENDA KUSOMA TENA CHUO KIKUU CHA OXFORD UINGEREZA