JWTZ MBEYA WAUA BAADA YA MWENZAO KUPIGWA NA WALINZI WA MADUKA


                                               Habari na Mwandishi wetu.
 Watu wawili wanadaiwa wamefariki dunia na wengine watatu wamejeruhiwa baada ya kupigwa na watu wanaodaiwa kuwa ni askari wa JWTZ.

Akiongea na Mtandao huu kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya DIWANI ATHUMAN amesema katika vurugu hizo mmtu mmoja ndiye aliyeripotiwa amefariki dunia hadi saa ambaye naye bado hajafahamika mara moja na kuongeza kuwa wengine watatu wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Ifisi Mbeya.

hata hivyo habari kutoka eneo la Tukio zinadai kuwa Novembeer 17 majira ya saa tano za usiku ktk eneo la DDC mbalizi walinzi wakiwa kwenye doria zao za maduka walimsimamisha askari mmoja wa JWTZ kisha kuanza kumpiga hali iliyopelekea maumivu makali na kukimbilia kwenye kituo cha polisi Mbalizi kwa ajili ya kutoa taarifa.

Badaa ya kufika ktk kituo hicho alipewa huduma mara moja ambapo askari hao waliondokana kwenda eneo la tukio na kuanza kufanya msako wa watu waliohusika hata hivyo usiku hawakufankiwa kumkamata hata mmoja.

siku inayofuata askari hao walifanikiwa kuwakamata walinzi watano na kuanza uchunguzi mara moja ambapo siku hiyohiyo majira ya saa tano za usiku askari wa JWTZ walivamia eneo hilo na kuanza kutembeza kipigo kwa wananchi waliokuwa eneo hilo ambapo kutokana na vurumai hizo watu wawili waliumia vibaya na wengine kujeruhiwa.

aidha watu hao walipelekwa ktk hospital ya Ifisi ambaopo majira ya saa 5 hiyo hiyo wawili kati ya hao waliokuwa wamepigwa walifariki dunia
 
Hata hivyo RPC DIWANI alisema kuwa uchunguzi unaendelea kwa ushirikiano wa Polisi na JWTZ kuwapata waliohusika na tukio hilo la uvunjifu wa sheria.
Chanzo: Chimbuko Letu Blog

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI