Akina mama waombolezaji wakisawazisha kaburi la marehemu Sinjembele Julius(62) aliyeuawa kwa kupigwa na mwanae Ndele Julius(25)

Baadhi ya waombolezaji wakishuhudia mazishi ya Sinjembele yaliyofanyika Nyumbani kwake katika kitongoji cha Igawilo kata ya Swaya Mbeya

UKISTAAJABU ya Musa utayaona ya firauni, unaweza kusema hadithi kumbe nikweli ,Mkazi wa Swaya jijini Mbeya Ndugu Ndele Julius amemuua mama yake mzazi kwa kumpiga mateke na ngumi kisha kutoroka pasipo julikana Novemba 25 mwaka huu.

Tukio hilo limetokea majira ya saa 10 jioni nyumbani kwa mama huyo mara baada ya kutokea kwa ugomvi kati ya mtoto wake na kijana mwingine hali iliyopelekea mama huyo kuingilia ndipo alipo kutwa na mauti huo.
Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoani humo Ndugu Diwani Athumani amesema kuwa Chanzo cha tukio hilo ni ugomvi uliokuwepo kati ya mtoto wake na kijana mwenzake kitendo ambacho kilipelekea mama huyo kuingilia ugomvi huo .

Amesema wakati mama huyo akijaribu kuamulia ugomvu huo mtoto wake alicha kupigana na mwenzake na kuanza kumshambulia mama yake kwa kumpiga ngumi na mateke mwilini.

Amesema mama huyo alifariki muda mchache kutokana na kupigwa sehemu mbalimbali za mwili wake na kusababishiwa majeraha makuibwa yaliyopeleka kupoteza uhai wake.

Awali akizungumzia tukio hilo Mtoto wa Kwanza wa mama huyo Ndugu Razaro Mbwiga amesema kuwa mdogo wake alikuwa na tabia ya kugombana na mama yake marakwamara .

Hata hivyo teyari mwili huo umekwisha chukuliwa hospitali na kuzikwa ambapo katika maziko hayo Chama cha Muungano wa kijamii (Mujata) umewataka vijana kujiepusha na vitendo viovu kama uvutaji bangi na pombe za kienyeji kwani ndio chanzo cha kutokea kwa vurugu nyingi. Mjengwa.





Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.