Ki-College Zaidi na NMB yawazawadia washindi 66

 Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Benki ya NMB, Stephen Chavallah (wa pili kulia) akibofya kitufe kwenye kompyuta kuwapata washindi wa promosheni ya Ki-College Zaidi na NMB wakati wa droo ya kwanza iliyochezeshwa Makao Makuu ya benki hiyo, Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkaguzi wa Michezo ya Kubahatisha, Humudi Abdulhusse na kutoka kushoto ni Meneja wa Amana, Boma Raballa na Meneja Masoko wa benki hiyo, Shilla Senkoro. Washindi 66 walipatikana.(PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
 Meneja Masoko wa NMB, Shilla Senkoro akionesha zawadi ya taa ya kutumia mionzi ya jua
 Shilla Senkoro aionesha kompyuta aina ya i pad atakayozawadia mwanafunzi Chacha Nyange Nchamcho na nyingine  Kelvin Gabone wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam , kila mmoja zawadi ya I Pad, katika promosheni ya Ki-COLLEGE Zaidi inayoendeshwa na benki hiyo.
Shilla Senkoro akionesha simu aina ya Samsung watakazo zawadiwa wanafunzi wawili walioshinda katika promosheni hiyo
BENKI ya NMB, leo imewazawadia wanafunzi wawili wa Chuo Kikuu Dodoma (UDOM), Chacha Nyange Nchamcho na Kelvin Gabone, kila mmoja zawadi ya I Pad, katika promosheni ya Ki-COLLEGE Zaidi inayoendeshwa na benki hiyo.

Promosheni hiyo inayohusisha wanafunzi wenye akaunti ya NMB Student, ilifanyika Makao Makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam, ambapo washindi wengine wawili walijishindia simu za mkononi aina ya Samsung Galaxy.

Jumla ya washindi 66 walipatikana katika droo hiyo, ambapo 60 kati yao walijishindia zawadi za taa maalum za kujisomea zinazotumia mionzi ya jua, fulana za NMB, jezi za Taifa Stars na ongezeko mara mbili la kaunti ‘Amana Maradufu.’

Akizungumza wakati wa promosheni ya kuwasaka na hatimaye kuwatangaza washindi hao, Meneja Masoko wa NMB, Shilla Senkoro, aliwataka wanafunzi kuendelea kufungua akaunti ya NMB Student au kuweka amana zao, ili kujishindia zawadi mbalimbali katika droo mbili zijazo.

Droo hiyo iliyochezeshwa chini ya Ofisa Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini, Humud Abdulhussein, ni ya Oktoba, ambapo washindi wa mwezi huu watasakwa mwezi ujao, huku wateja wa droo ya mwisho ya Desemba, watatafutwa Januari mwakani

Senkoro aliongeza kuwa, nia ya promosheni hiyo ni kurudisha sehemu ya faida yao kwa wateja, hususani wanafunzi kupitia akaunti maalum iliyoanzishwa mwaka 2007, kutokana na ongezeko la vyuo vya elimu ya juu nchini vilivyoongeza idadi ya wateja.

Alisema kuwa, hadi sasa akaunti ya NMB Student ina zaidi ya wanafunzi 70,000, waliofungua katika matawi mbalimbali nchini, huku akiwataka wengine kuendelea kujitokeza ili kujishindia zawadi zitakazotoa msukumo wa maendeleo yao kimasomo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*