Mahakama ya Rufaa yagoma kufuta rufaa ya Lema
Wakili Edson mbogolo akizungumza na waandishi wa habari nje ya jengo la Mahakama ya Rufaa
Aliekuwa Mbunge wa Arusha mjini, Godbles Lema akizungumza na wafuasi wake nje ya jengo la Mahakama ya Rufaa Tanzania
Aliyekuwa
Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), Godbles Lema (katikati) akitoka katika Mahakama ya
Rufaa huku akiandamana na wafuasi wake.Kwa hisani ya Habari Mseto Blog
Na
Happiness Katabazi
MAHAKAMA
ya Rufaa Tanzania, imekataa kuifuta rufaa iliyofunguliwa mahakamani hapo na aliyekuwa
Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), Godbles Lema kwa maelezo kuwa mapungufu yaliyopo kwenye
kikaza hukumu(decree) hayawezi kusababisha mahakama hiyo iifute rufaa
iliyokatwa na Lema inayopinga hukumu iliyotolewa mwaka huu na Mahakama Kuu
Kanda ya Arusha ambayo ilitengua ubunge
wake.
Uamuzi
huo mdogo ulitolewa jana katika Mahakama ya Rufani jijini Dar es Salaam,na
kuudhuliwa na umati wa wafuasi wa Lema na ulisomwa na Naibu Msajili wa mahakama
hiyo Zahara Maruma kwaniaba ya jopo la
majaji wanaosikiliza rufaa hiyo ambao wanaongozwa na Jaji Mkuu Othman Chande , Natalia Kimaro na Salum Massati.
Akisoma
uamuzi huo unaotokana na
pingamizi la awali lilowasilishwa na wajibu rufaa ambao ni wananchama wa
cha
Mapinduzi (CCM), jimbo la Arusha Mjini wanaotetewa na Medest Akida na
Alute Mughwai, dhidi ya mwomba rufaa(Lema) na Mwanasheria
Mkuu wa Serikali, Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Arusha mjini na
Mwanasheria Mkuu wa Serikali
anayewakilishwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali Timon Vitalis
wakati Lema akiwasilishwa Method
Kimomogoro na Tundu Lissu ambao jana hawakuwepo mahakamani na wakili
Edson
Mbogoro aliwawakilisha kwaniaba yao huku Mwanasheria Mkuu akiwakilishwa
na
mwanasheria wa serikali, Timon Vitalis.
Jaji
Chande alisema hivi karibuni wajibu
rufaa waliwasilisha pingamizi la awali ambapo waliwasilisha hoja tatu
ambapo
waliomba mahakama hiyo iifute alidai kuwa kikaza hukumu kilichotumiwa
na Lema kukata rufaa kilikuwa
hakina mhuri wa mahakama wala haionyeshi hukumu ya Mahakama Kuu Kanda ya
Arusha
iliyotengua ubunge wa Lema ilitolewa lini, kikaza hukumu
hakikuzingatia Kanuni za Masijala za Mahakama Kuu ya mwaka 2005 na
kwamba
kikaza hukumu hicho kilikuwa
kimekosekana maneno kama ‘hukumu hii imetolewa kwa mkono wangu’ na
kuomba rufaa
ya Lema ifutwe.
“Jopo
langu limepitia hoja za pande mbili limefikia uamuzi wa kukubaliana na hoja ya
kwanza kuwa ni kweli kikaza hukumu kilichotumiwa na Lema kukata rufaa mahakama
ya rufaa kilikuwa na dosari hizo ambazo ni hakikukwa na mhuri wa tarehe na tatizo hilo halikusababishwa na Lema ni
watendaji wa mahakama waliyoaanda Kikakaza hukumu hiyo;
“Kwa
sababu hiyo mahakama hii imekataa ombi la wajibu rufaa lilotaka mahakama hii
ifute rufaa iliyokatwa na Lema kwa sababu eti kikataa rufaa hicho kilikuwa na
mapungu hayo kwasababu licha ni kweli mahakama hii inakiri kuwepo kwa mapungufu
hayo, lakini mapungufu hayo hayawezi kufanya
mahakama hii iifute rufaa ya Lema.
“Na
hivyo basi mahakama hii imempatia Lema muda wa siku 14 kuanzia leo awasilishe upya
rufaa
yake ambayo atakuwa ameifanyia
marekebisho ambapo rufaa hiyo mpya
itapaswa ionyeshe ina mhuri na tarehe ya kutolewa kwa hukumu ya Mahakama Kuu
Kanda ya Dar es Salaam’alisema Jaji Chande.
Aidha Jaji Chande alisema jopo lake
limetupilia mbali hoja mbili za wajibu rufaa(makada wa CCM), zilizodai kikaza
hukumu hakikuzingatia Kanuni za Masijala
ya Mahakama Kuu ya mwaka 2005 na kwamba kilikosekana maneno kama ‘hukumu
imetolewa kwa mkono wangu’ , kwamba hoja hizo hazina mantiki kisheria na hivyo
inazitupilia mbali ”alisema Jaji Chande.
Uamuzi huu ni wa pingamizi la awali na hausiani na rufaa iliyokatwa na Lema
mahakamani hapo kwani rufaa iliyokatwa na Lema bado haijaanza kusikilizwa.
Oktoba 2 mwaka huu, pingamizi la awali
lilotolewa uamuzi wake jana lilianza kusikilizwa mjini Arusha,
wakili wa Lema, Kimogoro
alidai jaji Gabriel Rwakibarila wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kutoa
hukumu yake Aprili mwaka huu, ambayo ilitengua ubunge wa Lema, jarada
kesi hiyo liliamishiwa Dar es Salaam hivyo hakukuwa na muda wa
kupitia hukumu na hati ya kukazia hukumu hivyo kwani walikuwa wanaletewa
nyaraka hizo kutoka Dar.
“Waheshimiwa majaji wa Mahakama ya Rufaa,
wakili mwenzetu, Mughwai, ametueleza hapa aliomba mara mbili tofauti apewe tuzo
hiyo ikiwa imesahihishwa lakini hakupatiwa majibu, katika mazingira hayo
alitegemea sisi tungeipata vipi?” alihoji wakili huyo huku akielezea
kushangazwa na hatua ya mawakili wa wajibu rufaa kutowapa nakala ya barua hizo.
Akinukuu maamuzi mbalimbali ya
mahakama hiyo kuhusiana na masuala ya hati ya kukazia hukumu pamoja na kanuni
mpya za uendeshaji mashauri ya Mahakama ya Rufaa ya mwaka 2009, Wakili
Kimomogoro alidai kuwa si kila kikaza
hukumu hukumu chenye upungu kina fanya
rufaa iliyokatwa na mwomba rufaa kuwa batili.
Alidai kuwa hati ya kukazia hukumu iliyotumiwa na
mtejwa wake (Lema) kukata rufaa imekidhi vigezo vyote muhimu ikiwemo kuonyesha namba ya
kesi, majina na hadhi ya wadau, mambo yaliyokuwa yakidaiwa, imeainisha
kilichoamuliwa na mahakama pamoja na gharama.
Aliendelea kuieleza mahakama kuwa
hata jaji aliridhika nayo ndiyo maana aliamua kuisaini jambo alilosema kuwa
endapo jaji aliridhika kimakosa wao kama mawakili hawawezi kumfuata na
kumwambia hapa umeridhika vibaya hebu ridhika vizuri ili tukakate rufaa bali
wanachofanya wao ni kuendelea na hatua inayofuata ambayo ni kukata rufaa kama walivyofanya.
Hata hivyo Kimomogoro alidai kuwa suala la tuzo hiyo kutogongwa muhuri si
suala la jaji bali ni suala la utawala kwani anayegonga muhuri mara baada ya
jaji kusaini ni msajili wa mahakama.
Alidai kuwa makosa yaliyofanyika ni ya kawaida ambayo
hayaathiri kiini cha tuzo hiyo kwa kile alichoieleza mahakama kuwa tuzo haiwezi
kuwa batili kutokana na mchoro au mamlaka iliyoitoa bali kinachoangaliwa ni
maamuzi yaliyo ndani ya tuzo hiyo.
Aliomba mapingamizi hayo yatupwe kwa
gharama za wajibu rufaa kwani kasoro zilizojitokeza zinaweza kurekebishwa
wakati shauri hilo
likiendelea au kila upande ubebe gharama zake kwenye usikilizwaji wa
mapingamizi hayo kutokana na kuwa upande wa wajibu rufaa nao walishaandaa rufaa
panda.
Kwa upande wake wakili wa serikali
aliieleza mahakama hiyo kuwa anaunga mkono hoja za waleta rufaa huku akiweka
wazi kuwa hati ya kukazia hukumu hutolewa kwenye mashauri ya madai ambapo
alisema kuwa kazi ya kuweka muhuri si ya jaji bali ni ya masijala ya mahakama
kuu.
Baada ya uamuzi huo kutolewa jana ,Lema
alizungumza na wanachama wake na waandishi wa habari nje ya jengo la Mahakama
ya Rufaa Dar es Salaam, ambapo alianza kwa kusema ‘Peoples huku wafuasi wake wakiitikia Power’.
Lema alisema kwanza anawashukuru wanachama wa
Chadema Mkoa wa Dar es Salaam, kwa kuja kuudhulia mahakamani hapo na kusema
aliwasili jijini jana huku akiwa na wasiwasi mkubwa na uamuzi huo uliotolewa
jana na mahakama ya rufaa kwani kesi
mahakama iliaribiwa vibaya na mahakama
hivyo ndiyo maana jana alikuwa akisita kuja mahakamani hapo kuupokea
uamuzi huo kwasababu hivi sasa mahakama imekuwa na sifa mbaya hali
inayosababishwa wananchi wengine kuona hawawezi kupata haki zao.
“Nasema hivi kesi yangu iliaribiwa vibaya na
mahakama na ninamini rufaa hii niliyokata kama haitaingiliwa na mambo ya
kisiasa nitashinda rufaa yangu na
nitarejea bungeni kwa kishindo’ alisema Lema na kushangiliwa na umati.
Comments