MAKAMU WA RAIS KUFUNGUA MAONESHO YA NYUMBA DESEMBA 7-9
Mkurugenzi
wa Tanzania Homes Expo, Zenno Ngowi akizungumza na waandishi wa habari
kuhusu maonesho ya sekta ya nyumba yaliyoandaliwa na Kampuni ya Brand
Works. Kushoto ni Mratibu wa maonesho hayo, Rita Gedi na, Richard Mvula.
DAR ES SALAAM, Tanzania
MAKAMU wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal anatarajiwa kufungua
maonyesho ya taarifa sahihi za sekta ya nyumba yatakayojulikana kama Tanzania Homes Expo, yatakayofanyika Desemba 7
hadi 9 mwaka huu Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jijini Dar es Salaa leo, Mkurugenzi wa Tanzania Homes Expo, Zenno Ngowi amesema kuwa maonyesho hayo yameandaliwa na Kampuni ya Bland Works, Ngowi amesema kuwa
maonyesho hayo yanalenga kukuza sekta ya nyumba nchini kwa kukuza elimu ya umma
kuhusu aina mbali mbali za huduma zinazolenga sekta hiyo.
“Maonyesho haya tumekusudia kuwa jukwaa kuu la taarifa
zihusuzo makazi nchini Tanzania kwani yanatoa fursa kwa taasisi muhimu kama
manispaa zetu kuelezea wananchi mambo muhimu yahusuyo sekta hii kama
upatikanaji wa ardhi, vibali vya ujenzi
na mengineyo” alisema Ngowi.
Ngowi alisema kuwa maonyesho hayo yatatoa fursa kwa watoa
huduma za sekta hiyo kama mikopo, bima, wakandarasi, wachora ramani, makampuni
ya nyumba, makampuni ya ulinzi, marembo, vifaa vya ujenzi na mengine mengi
katika kupata nafasi ya kuelezea huduma wanazozitoa.
“Tunapenda kuwaalika makampuni binafsi na umma kushiriki
katika maonyesho haya muhimu kwani tumekusudia kufanya maonyesho haya mara moja
kila mwaka na tunaamini yataleta mafanikio katika kutatua kero za sekta hiyo”
alisema Ngowi.
Comments