Mapya Yaibuka Sakata La Mtuhumiwa Wa Mauaji Ya Mwandishi

Karandika  lililobeba mahabusu wengine likiwasili mahakamani hapo bila ya mtuhumiwa wa mauwaji ya Daudi Mwangosi
Askari  polisi  wakiweka ulinzi kumziba mwenzao asipigwe picha leo
Mtuhumiwa wa mauwaji ya aliyekuwa mwandishi  wa habari wa Chanel Ten mkoa  wa Iringa Daudi Mwangosi , askari mwenzao mwenye  namba G2573 Pasificus Cleophace Simoni (23) akiingia katika gari la polisi lenye namba za usajili PT 1404  huku ulinzi ukiwa umeimarishwa  kuzuia wanahabari  wasipige picha
Wanahabari  wakiwa  wamejipanga kwa  picha wakisubiri mtuhumiwa  kuletwa mahakamani hapo 
SAKATA ya mauwaji ya aliyekuwa  mwandishi  wa habari  wa  kituo cha Chanel Ten mkoani Iringa  marehemu  Daudi Mwangosi limeendelea  kuchukua sura mpya mkoani Iringa  baada ya askari  polisi  anayetuhumiwa kuhusika na mauwaji hayo kufichwa katika gari maalum na askari  wenzao .
Tukio  hilo  lilitokea  leo wakati mtuhumiwa huyo akifikishwa mahakamani huku askari  polisi hao  muda  wote  walionekana kuzunguka huku na kule katika mahakama hiyo kama njia ya  kuwathibiti  wanahabari  waliokuwepo mahakamani hapo wasipate nafasi ya  kumpiga  picha mtuhumiwa  huyo ambaye ni  askari mwenzao mwenye  namba G2573 Pasificus Cleophace Simoni (23)
Hata  hivyo  kabla ya kuingia karandika la mahabusu wengine gari ya polisi aina ya Toyota yenye namba  za usajili PT 1404 ikiwa na askari  zaidi ya 10 ilifika katika  viwanja  hivyo  vya mahakama na  kuegeshwa pembeni  bila ya mtuhumiwa  huyo aliyekuwa amefunikwa sura  yake kwa kofia na kufichwa kabisa sura  yake kuonekana  huku  akiwa amekaa mbele kwa dereva  huku akifichwa na askari mwenzake pasipo kushuka.

Zikiwa  zimebaki kama dakika  10 mahakama kuanza  gari  hilo lilisogea hadi mlango wa Mahakama na askari  waliokuwepo mahakamani hapo  zaidi ya 20 kulizunguka gari  hilo huku  wengine  wakiwathibiti  wanahabari akiwemo mwandishi wa habari hizi   kama njia ya kuzuia kupigwa picha kwa mtuhumiwa huyo. Baada ya  kuingia ndani ya mahakama, kabla ya hakimu kufika uthibiti ndani ya chumba cha mahakama ulikuwa mkali zaidi dhidi ya  wanahabari hasa  wale wenye kamera.
Wakati  huo  huo Mahakama ya hakimu mkazi wa  wilaya ya Iringa imeahirisha  kesi  hiyo ya mauwaji ya mwanahabari Daudi Mwangosi ambae pia alikuwa ni mwenyekiti klabu ya  waandishi  wa habari mkoa  wa Iringa (IPC), mtuhumiwa huyo askari mwenye namba G2573  Simoni (23) atafikishwa tena mahakamani hapo Desemba 5 mwaka huu kesi hiyo  itakapo tajwa  tena. 
Mwendesha mashitaka  wa jamhuri  Adolf Maganda  aliieleza mnahakamani  hiyo  mbele ya hakimu   Dyness Lyimo  kuwa mtuhumiwa huyo mnamo 02 Septemba mwaka huu katika kijiji cha Nyololo Wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa alimuua Daudi Mwangosi kwa makusudi kinyume na kifungu cha sheria namba 148 kifungu kidogo 5A.i cha makosa ya jinai.

Kwa mujibu wa kesi za jinai, sheria kifungu 196 kanuni ya adhabu Cap. 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002, kinakataza mtuhumiwa wa mauaji ya kukusudia kupewa dhamana.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*