Mh. Lukuvi awafariji maporoko waliojeruhiwa na majambazi Iringa

 Waziri  wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera), William Lukuvi ambaye ni mbunge  wa  jimbo la Isimani mkoani Iringa akimfariji  paroko wa parokia ya Isimani, Angelo Burgeo (60) na msaidizi wake Herman Myalla (36) waliolazwa katika  Hospitali ya mkoa  wa Iringa kwa matitabu zaidi baada ya  kuvamiwa na majambazi  juzi na kuporwa  fedha  zaidi ya shilingi Milioni 3.8 Picha na Francis Godwin


Na Francis Godwin,Iringa

KUFUATIA kuvamiwa  kwa makanisa matatu mkoani Iringa na kujeruhiwa kwa paroko  wa parokia ya Ismani mkoani Iringa Rais Dkt Jakaya Kikwete atoa  amfariji  paroko Angelo Burgeo (60) na msaidizi wake Herman Myalla (36)  waliojeruhiwa na majambazi  huku akiziomba taasisi  za dini  kutoa ushirikiano kwa  jeshi la polisi ili kuimarisha  ulinzi katika maeneo yao kama njia ya  kukomesha matukio ya ujambazi yanayofanyika katika maeneo ya taasisi za  dini.

Rais Dkt Kikwete alitoa wito  huo kupitia waziri  wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera), William Lukuvi ambaye ni mbunge  wa  jimbo la Isimani mkoani Iringa ambako paroko huyo na mwenzake  walivamiwa ,alitoa wito  huo  jana katika hospitali ya mkoa wa Iringa alipokuwa akiwasilisha salamu za Rais Jakaya Kikwete na kutoa pole kwa Paroko Angelo Burgeo (60) na msaidizi wake Herman Myalla (36) wa Kanisa Katoliki Parokia ya Isimani, wilayani Iringa.
Novemba 15, mwaka huu mapadri hao ambao wamelazwa katika hospitali ya mkoa wa Iringa wakiendelea na matibabu, walivamia na kushambuliwa kwa silaha za moto, mapanga na nondo na majambazi.
Watu watano wanaosikiliwa na polisi wakihusishwa na uhalifu huo katika tukio hilo ambalo mapadri hao mbali na kujeruhiwa vibaya waliibiwa zaidi ya sh Milioni 3.8.
Akiwasilisha salamu za Rais, Lukuvi alisema ametumwa kutoa pole kwa wahanga hao, waumini na viongozi wa dhehebu hilo la dini kwa ujumla wake.
“Tupo pamoja nanyi katika kipindi hiki kigumu ambacho majambazi wamekuwa wakiwavamia viongozi wa dhehebu hili la dini wakiamini mmehifadhi fedha na mali nyingine nyingi ndani ya parokia zenu,” alisema.
Alisema tukio la mapadri hao kuvamiwa na kujeruhiwa mkoani Iringa limekuja miezi michache baada ya matukio kama hayo kutokea katika parokia za Migori na Pawaga mkoani Iringa.
“Serikali imefanya kazi ya kutoa mafunzo kwa mgambo wengi karibu katika kila kijiji, ni wajibu wa taasisi hizi za dini kuwatumia hao au vinginevyo ikubali kushirikiana na jeshi la Polisi kutoa mafunzo kwa walinzi wao,” alisema.
Akipokea salamu hizo, Padro Burgeo alisema majambazi hao walifanikiwa kuingia ndani ya parokia yake baada ya kutumia lango la nyuma na kufanikiwa kuwapiga chenga walinzi wao.
Alisema katika tukio hilo ilikuwa afe lakini Mungu amesaidia kuyanusuru maisha yake baada ya kufikishwa mikononi mwa madaktari.
Kaimu wa Mganga Mkuu wa Mkoa Dk Faustine Gwanchele alisema baada ya kumfanyia upasuaji na kutoa risasi tatu kwa Padri Burgeo hali yake inaendelea vizuri pamoja na kusumbuliwa na ugonjwa wa kisukari

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.