MICHAEL YOMBAYOMBA KUPAMBANA NA SAID OMAR 'GOGO POA' KUCHANGIA WAGOJWA WA MOYO

 Saidi Omari 'Gogo Poa' .kushoto na Rajabu Mhamila'Super D'


 



MABONDIA wazamani walioiletea nchi Medali katika mashindano ya All Africa Games na Jumuiya ya Madola miaka ya 1998, Michael Yombayomba na Said Omari 'Gogo Poa' wamejitolea kupanda ulingoni kutwangana kwa ajili ya kuchangia watoto wenye matatizo ya Moyo.

Yombayomba, ambaye alitwaa medali ya dhahabu katika mashindano ya Jumuia ya Madola katika miaka hiyo ya 1998 na Gogo Poa wameamua kutwangana ikiwa ni sehemu ya mchango wao kwa watoto hao huku wakisisitiza wadau kuunga mkono tukio hilo. 

Akizungumza na gaazeti hili Gogo Poa alisema pambano hilo litafanyika Januari 25 mwakani ambapo pia litasindikizwa na mapambano ya mabondia mbalimbali wenye viwango vya juu nchini. 

"Tumeguswa sana na tatizo hili la watoto wanaougua ugonjwa wa moyo ambao wengi wao hukosa fedha kwa ajili ya matibabu hivyo sisi kama sehemu ya jamii tutahamasisha uchagiaji wa fedha kwa kujitolea kupanda ulingoni na chochote kitakachopatikana itakuwa ni sehemu ya mchango wetu,"alisema Gogo Poa.

Aliwaomba wadhamini na wadau mbalimbali kujitokeza kuzamini mchezo huo ambao una tija ya kuchangia watoto hawo kwani ata wao walikuwa watoto ndio mana wamekuwa katika afya nzuri na kucheza mchezo huo na kuiletea sifa taifa hili kwa kuleta Medali

Hivyo na watoto hawo wanatakiwa wawe na Afya njema ili wapate kuja kurithi nyayo zetu bila afya ya mtoto michezo yote akuna kwa kuwa vipaji vingi vinangaliwa ukiwa mtoto

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA