MSONDO NGOMA KUZINDUA VYOMBO VIPYA

BENDI Kongwe ya mziki wa dansi nchini Tanzania Msondo Music inatarajia kuzindua vyombo vyake vipya kabisa walivyokabidhiwa hivi karibuni na Kampuni ya KONYAGI akizungumza na waandishi wa habari msemaji wa bendi hiyo Rajabu Mhamila 'Super D' amesema tumeshapewa vyombo na Konyagi ambavyo tutavizindua mbele ya mashabiki wetu siku ya Ijumaa pale LIDAZ CLUB siku ya Ijumaa hivyo wapenzi wote wa bendi ya Msondo mnaombwa kuhudhuria kwa wingi ili kuona vyombo vipya

Pamoja na kupata burudani za bendi hiyo zikiwemo nyimbo za zamani na za sasa kwa ajili ya kuanza wik end Super D aliongeza kwa kusema wapenzi watakaokuja siku hiyo watapata burudani za radha tofauti tofauti kwani wamepanga kukonga nyoyo za mashabiki wao kwa kutumia vyombo vyao vipya

Bendi hiyo siku ya Jumapili itamaliza burudani za wik end katika ukumbi wa Max Bar Ilala bungoni




Mkurugenzi wa Bendi hiyo Muhidini Maalimu Gulumo ataongoza kundi zima la wana msondo ngoma akiwemo Said Mabera,Shabani Dede, Romani Mn'gande, Eddo Sanga, Juma Katundu, Hassani Moshi na wendine kibao kwa ajili ya kuwaburudisha mashabiki

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

GSM ARIDHIA UJENZI WA UWANJA WA YANGA JANGWANI

WACHEZAJI YANGA WAGOMA KABISA KUFANYA MAZOEZI LEO, LWANDAMINA AIBUKA PEKE YAKE SHAMBA LA BIBI

DKT. MAJULE AMFANYIA MAPOKEZI MAKUBWA BALOZI WA CHINA NCHINI

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

Wasifu wa Kizza Besigye

HERSI KWENDA KUSOMA TENA CHUO KIKUU CHA OXFORD UINGEREZA