MTOTO WA MIAKA MITATU ACHOMWA MOTO KISHA KULAZIMISHWA KULA KINYESI CHAKE MAJENGO JIJINI MBEYA

MTOTO ANETH AKIWA AMEOKOLEWA NA WASAMARIA WEMA HUKO MAJENGO

HIVI NDIVYO ALIVYOUNGUZWA MTOTO ANETH NA MAMA YAKE MDOGO

HUYU NDIYO MAMA MDOGO WA ANETH AMEJULIKANA KWA JINA LA BAHATI LUKANGARA NDIYO ALIYEMUUNGUZA MTOTO ANETH


HAPA MAJIRANI WAKIJARIBU KUMUULIZA SABABU ZA KUMUUNGUZA HUYO MALAIKA WA MUNGU NINI SABABU YAKE MPAKA AKACHUKUA HATUA YA KUMUUNGUZA LAKINI KWA KIBURI CHA HUYO MAMA ALIKAA KIMYA KABISA BILA YA KUJIBU CHOCHOTE

MWENYEKITI WA MTAA HUO HABIBA MWAKITALU AMEMBEBA MTOTO ANETH TAYARI KWA KUMPELEKA HOSPITALI HUKU NYUMA AKIFUATIWA NA MWESHIMIWA DIWANI KATA YA MAJENGO SAMWELI

WANANCHI WENYE HASIRA KALI WALIMCHUKUA MAMA HUYO NA KUMPELEKA KITUO CHA POLISI


MTUHUMIWA NA MGONJWA WANAINGIZWA KATIKA GARI LA MWESHIMIWA DIWANI TAYARI KWA KUPELEKWA POLISI

Katika hali isiyo ya Kawaida Mkazi wa majengo jijini Mbeya Ndugu Bahati Rukangara amemchoma moto mtoto mdogo wa mika 3 aliyefahamika kwa jina la Aneth kisha kumfungia Ndani na kumlazimisha ale kinyessi chake.

Akizungumza Mwenyekiti wa mtaa huo Ndugu Habiba Mwakitabu amesema kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa 10 :30 asabuhi ambapo majirani na mwanamke huyo waligundua mara baada ya kusikia sauti ya mtoto huyo akilia kutokana na maumivu.

Amesema mara baada ya kusikia sauti hiyo walifika eno hilo na kunza kumhoji ili kufahamu kiini cha tatizo hilo ambapo alishindwa kutoa ushirikiano ndipo walipo anza kumpiga .
Amesema kutokana na hali hiyo majirani walilazimika kubomoa mlango ndipo walipo mkuta mtoto huyo akiwa uchi huku ameungua vibaya mwilini hasa katika upande mmoja eneo la mkono wa kushoto .

Amesema mara baada ya kumhoji mtoto huyo aliwaeleza kuwa mama yake mdogo alichukua nguo na mkumfunga mkononi kisha kumwagia maji ya moto pamoja na kumlazimisha ale kinyesi chake hali ambayo iliwafanya washindwe kuvumilia na kuanza kupiga kelele kwa lengo la kuomba msaada kwa watu wengine.

Kwa mujibu maelezo ya mwenyekiti huyo amesema kuwa Mtuhumiwa huyo amekuwa akifanya vitendo vya manyanyaso kwa mtoto huyo marakwamara ambapo wamekuwa wakimuonya lakini amekuwa si mtu wa kusikia.
Ameesema mtoto huyo si wa kwa kwakwe kwani amekuwa akiishi naye kwa muda mrefu sasa ambapo aliachiwa na dada yake ambaye hakufahamika kuwa nayishi wapi kwa sasa.

Hata Diwani wa kata hiyo Ndugu Samuel Mamboma alifika eneo hilo tukio na kutoa msaada wa usafiri kwa lengo la kumfikisha mama huyo polisi pamoja na mtoto huyo ambaye naye alikimbizwa Hospitali.
Hata hivyo amesema tukio hilo si la kwanza kutokea katika meaeno hayo kwani kumekuwepo na matukio mengi hasa ya utoaji mimba na kutupwa watoto.

PICHA KWA HISANI YA KALULUNGA
HABARI KWA HISANI YA EMANUEL MADAFA

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI