MWENYEKITI WA CCM RAIS KIKWETE AKAGUA KIWANJA CHA MAKAO MAKUU YA CHAMA, UKARABATI WA KUMBI ZA MIKUTANO DODOMA


 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo juu ya ukarabati wa ukumbi wa mikutano wa 'White House' ulio katika makao makuu ya CCM mjini Dodoma ambao unafanyiwa ukarabati mkubwa ili kukidhi mahitaji ya sasa. Rais Kikwete alisimama kwa muda mjini Dodoma siku ya Jumanne Novemba 6, 2012 akitoka katika ziara ya kikazi mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Singida alikokagua jumla ya miradi 19 ndani ya wiki moja. PICHA NA IKULU
 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua maandalizi ya ukumbi utaotumika wakati wa mkutano Mkuu wa CCM ulio kitongoji cha Kizota mjini Dodoma. Rais Kikwete alisimama kwa muda mjini Dodoma siku ya Jumanne Novemba 6, 2012 akitoka katika ziara ya kikazi mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Singida alikokagua jumla ya miradi 19 ndani ya wiki moja.
 Mafundi rangi wakiwa kazini kuweka mambo sawa nje ukumbi utaotumika wakati wa mkutano Mkuu wa CCM ulio kitongoji cha Kizota mjini Dodoma
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongiozi wengine wakipata maelezo toka kwa Katibu Mkuu wa CCM Bw. Wilson Mukama juu ya maandalizi ya ujenzi wa makao makuu na vitega uchumi wa chama hicho mjini Dodoma ambako alisimama kwa muda siku ya Jumanne Novemba 6, 2012 akitoka katika ziara ya kikazi mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Singida alikokagua jumla ya miradi 19 ndani ya wiki moja.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

GSM ARIDHIA UJENZI WA UWANJA WA YANGA JANGWANI

WACHEZAJI YANGA WAGOMA KABISA KUFANYA MAZOEZI LEO, LWANDAMINA AIBUKA PEKE YAKE SHAMBA LA BIBI

DKT. MAJULE AMFANYIA MAPOKEZI MAKUBWA BALOZI WA CHINA NCHINI

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

Wasifu wa Kizza Besigye

HERSI KWENDA KUSOMA TENA CHUO KIKUU CHA OXFORD UINGEREZA