MZEE WA UPAKO NI ZAIDI YA MAMLAKA YA HALI YA HEWA

Wakati mwingine Mamlaka ya Hali ya Hewa inawapa sifa za bure baadhi ya watu kutokana na kushindwa kwake kuwa na utabiri wa kisayansi. Itakumbukwa kuwa Mamlaka iliposema kutakuwapo mvua za El Nino, Mzee wa Upako; akatangaza kwa kuapa kabisa kwamba endapo mvua hizo zingenyesha, basi angeacha kuhubiri! Kweli, mvua hizo zimepotea, na sasa Mamlaka inathibitisha kuwa hazipo!!

Hatari ninayoiona hapa ni kwamba wananchi watakuwa na imani zaidi na wachungaji (hata kama wamo waongo) kuliko Mamlaka inayoendeshwa na wanasayansi! Pengine ni muhimu basi, Mamlaka kutofuja fedha kwa kwenda Nairobi kwenye mkutano ulioandaliwa, badala yake wamfuate Mzee wa Upako ili awaeze hiyo hali ya "hewa isiyokuwa ya kawaida" maana yake ni nini, na itakuwa na athari gani? Nashauri hiyo kwa sababu inaelekea maono yake ni zaidi ya utabiri wa wanasayansi wetu.

Haitashangaza kuona Kanisa la Mzee wa Upako likijaa hadi pomoni kutokana na "utabiri" wake huu ambao umekuwa wa kweli kuliko wa Mamlaka ya Hali ya Hewa.

Nawasilisha.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

GSM ARIDHIA UJENZI WA UWANJA WA YANGA JANGWANI

WACHEZAJI YANGA WAGOMA KABISA KUFANYA MAZOEZI LEO, LWANDAMINA AIBUKA PEKE YAKE SHAMBA LA BIBI

DKT. MAJULE AMFANYIA MAPOKEZI MAKUBWA BALOZI WA CHINA NCHINI

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

Wasifu wa Kizza Besigye

HERSI KWENDA KUSOMA TENA CHUO KIKUU CHA OXFORD UINGEREZA