NASSIB RAMADHANI NA FRANCIS MIYAYUSHO KUGOMBANIA UBINGWA WA WBF SIKU YA UHURU WA TANGANYIKA
| ||||
Mabondia
Nassibu Ramadhani na Fransic Miyayusho wakitunishiana misuri wakati wa
kutambulisha mpambano wao wa ubingwa wa WBF utakaofanyika Desemba 9
katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam Na Richard Mwaikenda MABONDIA Francis Miyeyusho na Nasib Ramadhan wana kupambana Siku ys Uhuru kwenye Ukumbi wa PTA, viwanja vya Sabasaba, Dar es Salaam, kuwania mkanda wa ubingwa wa Mabara wa Shirikisho la Ngumi Duniani (WBF). Akizunguza katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Kampuni ya Darworld Links Ltd, inayoratibu pambano hilo, Mohamed Bawazir alisema mabondia hao mahili wataoneshana umwamba kwa raundi 12. Alisema wapenzi wa mchezo huo watafaidika zaidi kwa kushuhudia mapambano matano makali ya utangulizi. Aliwaja watakaotwangana katika ni utangulizi; Fadil Majia dhidi ya Juma Fundi (raundi 8), Mohamed Matumla na Doi Miyeyusho (raundi 6), Ibrahim Class dhidi ya Said Mundi (raundi 8), Fred Sayuni na Deo Samwel (raundi 6) na Hassan Kidebe dhidi ya Baina Mazola (raundi 6). Mabondia hao walipata wasaa wa kutambiana ambapo, Ramadhan aliwaomba wapenzi wa mchezo huo kutokosa kushuhudia wakati akimwadhiri vibaya kaka yake Miyeyusho. Miyeyusho alimuonya mdogo wake huyo, kukubali kupigana na yeye ni sawa na kudandia mbele ya treni lililoko kwenye mwendo, ambapo madhara yake ni kukanyagwa, hivyo wapenzi wa ndondi wategemee kuona jinsi atakavyomchakaza. Pambano hilo litakalosimamiwa na Shirikisho la Masumbwi Tanzania (PST), linadhaminiwa na JB Belmont Hotel, gazeti la Jambo Leo na Kituo cha Redio cha Times Fm. |
Comments