Nyalandu Ataka Ubora Chuo Cha Taifa Cha Utalii


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu (wapili kutoka kulia) akimsikiliza kwa makini Kaimu Mkurugenzi wa Mafunzo, Naiman Mbise alipokuwa akimuelezea matumizi ya majiko ya kisasa yatakayotumika kufanyia mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi Chuo cha Taifa cha Utalii kilichopo mtaa wa Garden Avenue na Shaaban Robert mkabara na Chuo cha IFM na Makumbusho ya Taifa na nyumba ya Utamaduni alipotembelea chuo hicho jana.

Na: Tulizo Kilaga
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu ameutaka uongozi wa Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) kuhakikisha chuo hicho kinatoa elimu yenye ubora wa kimataifa.
Aliyasema hayo Dar es Salaam jana alipotembelea jengo jipya la Chuo cha Taifa cha Utalii lililopo mtaa wa Garden Avenue na Shaaban Robert mkabara na Chuo cha IFM na Makumbusho ya Taifa na nyumba ya Utamaduni kwa mara ya kwanza kuona shughuli zinazofanywa na chuo hicho.
Mhe. Nyalando alisema chuo hicho ambacho kina vifaa vya kisasa, kitakuwa na mafanikio zaidi na kutambulika duniani kote na kuijengea heshima Tanzania iwapo mitaala yake itazingatia zaidi viwango vya kimataifa.
“Tanzania tunatatizo lakutokuwa na watu waliobobea katika tasnia ya utalii, kwa chuo hichi cha kisasa hatuna budi kupanua wigo kwa kuhakikisha mafunzo mengine yanaongezwa bila kusahau masuala ya lugha za kigeni kwa kuzingatia ubora na viwango vinavyotambulika kimataifa na hivyo kuvutia wanafunzi kutoka ndani na nje ya nchi na hata wadau wa sekta ya utalii nchini kuwapa ajira wahitimu,” alisema Mhe. Nyalando ambaye pia ni mdau wa sekta ya utalii.
Alisema lengo la Serikali na Wizara ni kuhakikisha chuo hicho kinakuwa miongoni mwa vyuo bora Barani Afrika chenye kuzalisha wahitimu wanaotambulika kimataifa. Hivyo kuwa na sifa yakufanya kazi hata akitoka nje ya mipaka ya nchi.
Waziri Nyalandu alisema Wizara itahakikisha wakufunzi wa chuo hicho wanapewa nafasi za kwenda kusoma kwenye vyuo vya nje ili kuongeza ujuzi, kutoa kipaumbele katika mgao wa fedha ili kukipa uwezo wa kutanua wigo wa mafunzo yake na kukipa uhuru binafsi wa kiutawala ili suala la ajira liishie kwenye bodi.
Naye Kaimu Mtendaji Mkuu wa Chuo hicho, Rosada Msoma, alisema chuo hicho kinatoa kozi za miaka miwili kwa ngazi ya Astashahada na Stashahada na tayari kimeanza na wanafunzi 171 ambao wanajifunza masuala ya Uzalishaji Chakula, Uokaji, Uandaaji wa Chakula na Vinyaji, Uandaaji wa Vyumba, Mapokezi, Ugawaji Vyumba na Sanaa ya Mapishi.
Alisema chuo hicho kimejipanga kuhakikisha wahitimu wake wanakuwa bora katika soko la ajira kwa kuweka msisitizo kwenye elimu ya nadhalia na vitendo, na tayari chuo kimeanzisha maeneo ya kitalii yaliopo katika jiji la Dar es Salam kwa ajili ya Safari za jiji zitakazoongozwa na wanafunzi wanaosoma masomo ya Uongozaji Watalii.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.