RAIS KIKWETE ASISITIZA USHIRIKANO SIPO II.





Na Zawadi Msalla - MAELEZO
Arusha.
Rais Jakaya Kikwete ameiasa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi Kusini mwa Afrika (SADC) kuimarisha ushirikiano kati yake na nchi wanachama wa Jumuiya hiyo ili kufanikisha utekelezaji wa Mkakati wa pili wa kushughulikia masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama wa Jumuiya hiyo.
Rais Kikwete ameeleza hayo wakati akizindua Mkakati wa kushughulikia masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama wa Jumuiya hiyo (SIPO II) jijini Arusha wakati wa mkutano uliowahusisha wawakilishi mbalimbali kutoka katika Jumuiya wanachama wa SADC.
Amesema ili malengo ya Mkakati huo yaweze kufanikiwa ni lazima ushirikiano wa ndani na nje wa nchi hizo wanachama uimarishwe na kuongeza kuwa SADC haiwezi Kutegemea mikakati ya ndani ya ulinzi na Usalama ya nchi fulani kutaka kutekeleza mkakati wake.
"SADC haitakiwi kuiingilia kwa kutaka kuibadili mikakati ya ndani ya Nchi wanachama ya ulinzi na usalama badala yake washirikiane kwa karibu kuangalia nini cha kufanya" Amesema Rais.
Kuhusu umuhimu wa mkakati huo Rais Kikwete amesema utakuwa muongozo wa SADC katika masuala yote ya ulinzi, usalama na siasa, na umejikita katika kutatua vikwazo mbalimbali vya kiulinzi vilivyopo.
Amefafanua kuwa Utekelezaji wa SIPO na maazimio yake utapelekea hali ya amani na utawala bora kwa Nchi nyingi za Afrika na kuongeza kuwa katika awamu ya pili ya SIPO mabadiliko mengi yamefanyika yakiwemo uongezaji wa vipaumbele katika mfumo wa utekelezaji na ufuatiliaji wa masuala ya ulinzi na usalama.
Uzinduzi wa SIPO II utaangalia ushirikiano kati ya Nchi wanachama, ushirikiano katika masuala ya kibiashara, uhakika wa kushughulikia masuala ya upatikanaji wa Amani na ushirikiano katika nyanja ya habari.
Akieleza historia ya chombo cha Usalama cha SADC alisema kabla ya kuanzishwa kwa chombo hicho kulikuwa na ushirikiano wa nchi katika masuala ya ulinzi na usalama na kubainisha kuwa kuanzishwa kwa SIPO kunatokana na nchi wanachama kuona umuhimu wa kuwa na chombo kinacho waongoza katika masuala hayo yote.
Awali akizungumza na wajumbe wa mkutano huo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Benard Membe amesema kuwa SIPO imekuwa ni nyenzo muhimu nay a kutegemewa na nchi za SADC katika masuala yote ya usalama.
Amesema SIPO ilizinduliwa rasmi mwaka 2004 na baadae kufanyiwa marekebisho ya kimsingi mwaka 2007 na kueleza kuwa kutokana na marekebisho hayo ya Mwaka 2007 ilikubaliwa kuwa mikakati na vapaumbele vya SIPO iwe inapitiwa kila baada ya miaka mitano.
Aidha uzinduzi huo utafuatiwa na mafunzo mbalimbali yatakayoendeshwa na wataalamu kwa muda wa siku nne

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI