SUNZU AMALIZA MKATABA SIMBA SC, KASHESHE KUMUONGEZEA

Felix Sunzu Jr. kushoto alipokuwa akisaini mkataba wa awali na Simba, ambao unamalizika mwezi ujao. Kulia ni Katibu wa Simba SC, Evodius Mtawala

Na Mahmoud Zubeiry
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Zambia, Felix Mumba Sunzu Jr. anatarajiwa kumaliza mkataba wake mwezi ujao katika klabu ya Simba SC na hadi sasa mustakabali wake haueleweki kama ataongezewa mkataba au la. 
Kumekuwa na mawazo tofauti ndani ya Simba SC kuhusu Sunzu, ambaye kwa sasa ndiye mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi Tanzania, Sh Milioni 5, kwamba hachezi kwa kiwango cha fedha anazolipwa.
Lakini wengine wanaamini Sunzu anawajibika vizuri na anastahili kwa fedha anayolipwa. Pamoja na hayo, hali ya kiuchumi ndani ya klabu hiyo kwa sasa, inatia shaka kama itaweza kuurudia mkataba ule ule wa Sunzu.
Kwa kawaida, baada ya kumaliza mkataba, Simba ili kuendelea kuishi na Sunzu, italazimika kumpa fedha ya dau la usajili, ambalo kwa mwaka haliwezi kuwa chini ya dola za Kimarekani 15,000 (zaidi ya Sh. Milioni 20 za Tanzania) na kukubaliana kuhusu mshahara uwe ule ule au mpya.
Kulingana zengwe lililotawala juu ya dola za Kimarekani 3,500 anazolipwa Sunzu kuna uwezekano Simba ikataka kuuteremsha mshahara huo, hasa ikizingatiwa kuwa, kwa sasa hakuna taarifa zozote za Mzambia huyo kutakiwa na timu, iwe ndani ua nje ya nchi.  
Kumalizika kwa mkataba wa Sunzu ni mtihani mwingine kwa Simba, ambayo kwa sasa inakabiliwa na kasheshe la kuingia mkataba mpya na mshambuliaji wake Mganda, Emmanuel Okwi ambaye yuko vizuri kisoka na anatolewa macho na Azam na Yanga.
Na suala la usajili linazidi kuwa zito kwa sababu Kamati ya Utendaji ya Simba SC wiki hii imevunja Kamati zote ndogondogo, ikiwemo Kamati ya Usajili, iliyokuwa chini ya Mwenyekiti Zacharia Hans Poppe. Chanzo; Bin Zubeiry Blog

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI