TUME YA HAKI ZA BINADAMU (THBUB) YAZITAKA TAASISI ZINAZOSIMAMIA SHERIA KUZINGATIA HAKI


Mwenyekiti wa Tume Ya Haki za Binaadamu na Utawala Bora Jaji Kiongozi (Mstaafu) Amiri Ramadhan Manento kulia na Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo Mahfoudha Hamid 

DAR ES SALAAM, Tanzania

TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora imezitaka taasisi zinazosimamia sheria nchini kuhakikisha zinazingatia haki za binadamu na misingi ya utawala bora ili haki iweze kupatikana  kwa wakati na kwa watu wote. Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam jana, na Kamishina wa Tume hiyo, Bernadeta Gambishi, wakati alipokuwa  akizindua mradi vitabu (Vitini),vya  maboresho ya sheria. Alisema kwa kuzingatia hayo kunaweza kuharakisha  upatikanaji wa haki katika makundi yote ya kijamii nchini, kusimamia maadili na uweled wa maofisa wa sheria, pia ukuzaji wa uhuru wa mahakama.

Gambishi alisema kimsingi mradi huo una malengo makuu sita ambayo yatatekelezwa kwa kupitia mkakati wa Kati.

 Akiyataja baadhi maeneo hayo, kuwa ni pamoja na Mfumo bora wa sheria kitaifa: lengo hilo linasimamiwa na Tume ya kurekebisha sheria nchini kwa kushirikiana na taasisi nyingine washirika. Haki za  Binadamu na usimamizi wa haki hili linasimamiwa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na upatikanaji wa haki kwa walio na uwezo mdogohilo linasimamiwa na Taasisi zisizo za Kiserikali (NGO’S), mfano mmoja ni Chama cha Wana Sheria Nchini (TLS). Naye Kaimu Mkurugenzi wa Sheria, Reginald Makoko, alisema bado Watanzania wengi wanakabiliwa na uwelewa mdogo wa sheria hali inayowafanya baadhi yao kupoteza haki zao. Hata hivyo, tatizo hilo kwa sasa limepungua kutokana kuwepo kwa vyama vyama vya kisheria ambavyo vinatoa msada wa kisheria bure , malalamiko mengi kuwasilishwa huko.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.