THE
UNITED REPUBLIC
OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
|
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
Fax: 255-22-2113425 |
![]() |
PRESIDENT’S OFFICE,
THE
STATE HOUSE,
P.O. BOX
9120,
DAR
ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
akagua miradi 19 katika wiki moja
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amerejea Dar
es Salaam mchana wa leo, Jumanne, baada ya kumaliza
ziara ya siku tisa katika mikoa minne ambako amekagua, kuanzisha ama kuzindua
miradi 19 ya maendeleo na kutembea kiasi cha kilomita 2,770.
Rais
Kikwete amewasili Dar es Salaam akitokea Dodoma
ambako amefanya ziara ya kikazi ya siku mbili baada ya kumaliza ziara katika
mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Singida.
Katika
Mkoa wa Kilimanjaro ambako Rais Kikwete alianzia ziara yake Oktoba 28, mwaka huu,
miongoni mwa mambo mengine alikagua nyumba za wahanga wa maporomoko ya mwaka
2006 kwenye kijiji cha Goha na akafungua Kiwanda cha Kusindika Tangawizi
kilichoko Mamba Miamba, Wilaya ya Same, na akafungua Shule ya Sekondari ya Kata
ya Asha Rose Mingiro iliyoko mjini Mwanga.
Miradi
mingine aliyoifungua Rais Kikwete katika Mkoa wa Kilimanjaro ni uzinduzi wa
barabara za Rombo Mkuu-Tarakea na Kwasadallah-Masama na akafungua Ofisi ya Mkaguzi
Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (NAO)
mjini Moshi.
Katika
Mkoa wa Arusha, Rais Kikwete alizindua Hospitali ya Wilaya ya Arusha ya
Olturumet, akazindua Mradi Mkubwa wa Uboreshaji wa Miji kwa kufungua barabara
za Jiji la Arusha, akazindua Jiji la Arusha, akafungua rasmi Chuo Kikuu cha
Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela na akatembelea Kiwanda cha Nguo cha
A-Z.
Kabla
ya kuondoka Mkoani Arusha, Rais Kikwete alifungua Shule ya Msingi ya Sokoine na
kuzindua ukarabati mkubwa wa Barabara ya Minjingu-Arusha.
Mkoani
Manyara, Rais Kikwete alifungua rasmi Barabara ya Singida-Minjingu-Arusha,
akazindua mradi mkubwa wa maji wa Mji wa Babati na akaweka jiwe la msingi
kwenye ujenzi wa Barabara ya Babati-Bonga.
Mkoani
Singida, Rais Kikwete alizindua mradi mkubwa wa maji wa Mwankoko kwa ajili ya
Mji wa Singida, akaweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa Barabara ya
Manyoni-itigi-Chaya na akafungua Barabara ya Issuna-Manyoni.
Imetolewa na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
6
Novemba, 2012

Comments