WANASACCOS 400 WA UVIMA-WAMA WAJIUNGA NHIF

 Mkurugenzi wa Uwezeshaji Wananwake wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Tabu Likoko akiwahamasisha wanawake wa Umoja wa Vikundi vya kuweka na Kukopa (UVIMA), wakati wa hafla ya wanachama wa wa umoja huo kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Majohe, Ilala, Dar es Salaam leo.
 Ofisa Mawasiliano na Elimu kwa Umma wa NHIF, Grace Kisinga (kushoto), akiwaelekeza Lwiza Libanja (kulia) na  Rose Furaha, jinsi ya kujaza fomu ya kujiunga na mfuko huo.

 Ofisa Mawasiliano Mwandamizi wa NHIF, Luhende Singu akigawa kalamu kwa wanachama wa Uvima.
 Meneja Uanachama wa NHIF, Ellenntruda Mbogoro akiwaelekeza wana Uvima jinsi ya kujaza fomu za uanachama wa kujiunga na mfuko huo.

Baadhi ya wanachama wa Uvima wakiandikishwa kujiunga na mfuko huo.
Mkurugenzi wa Operesheni wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Eugen Mikongoti akielezea faida ya kujiunga na mfuko huo, wakati wa kuwaandikisha sehemu ya wanachama 400 wa  Muungano wa vikundi vya kuweka na kukopa (UVIMA),  eneo la Majohe, Ilala, Dar es Salaam. Vikundi hivyo vinafadhiliwa na Taasisi ya  Wanawake na Maendeleo (WAMA). Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Uvima, Tatu Mgao na Mkurugenzi wa Idara ya Uwezeshaji Wanawake wa WAMA, Tabu Likoko.
 Mwenyekiti wa Muungano wa vikundi vya kuweka na kukopa (UVIMA), Tatu Mgao (kulia), akitoa shukurani kwa WAMA na NHIF kuwawezesha wanachama wa umoja huo kujiunga na masuala ya matibabu ya mfuko huo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), Athuman Rehani, Mkurugenzi wa Operesheni wa NHIF, Eugen Mikongoti  na Mkurugenzi wa Uwezeshaji Wanawake wa WAMA, Tabu Likoko.
 Wanachama wa Uvima wakishangilia baada ya kutangaziwa na uongozi wa NHIF , wamekubaliwa kujiunga na mfuko huo ambapo watakaonufaika kwa kulipia ada ya sh. 10,600 kwa mwezi ni watu sita, ambao ni mama, baba na watoto wao wanne.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.