WATAKA MAFISADI WANYONGWE

Wananchi wakichangia mabadiliko ya Kaiba Mpya
WAKAZI wa Tarafa ya Lupembe, Mkoa wa Njombe wamesema wanataka Katiba mpya itamke viongozi ambao watatambulika kuwa mafisadi, wapewe adhabu ya kunyongwa.
Licha ya pendekezo hilo, walisema wanataka watu watakaobainika kuwapa wanafunzi wa kike mimba, wapewe adhabu ya kufungwa jela miaka 30 na kuchapwa bakora 12 wakati wakuingia jela na kutoka.
Wakitoa maoni yao juzi kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, walisema mtu akiwa fisadi ni wazi anataka kuwaua wananchi kwa kuwafanya waendelee kuwa maskini.
Alfred Sanga (50), alisema kiongozi akiwa fisadi ni wazi anataka kuwaua wananchi kwani anasababisha wakose mahitaji yao muhimu ya binadamu.
Sanga alisema wananchi wengi wanalalamika maisha magumu kwa kukosa fedha, lakini baadhi ya watu wanahujumu uchumi kwa kujilimbikizia mali jambo ambalo siyo jema.
“Nataka Katiba mpya iseme kwamba kiongozi fisadi atapewa adhabu ya kunyongwa, kwani huyo hawatakii mema wananchi,” alisema Sanga na kuongeza:
“Haiwezekani wananchi kila siku wanapiga kelele maisha magumu, halafu watu wachache wanajinufaisha wenywe kwa kumiliki majumba ya kifahari, magari, kutibiwa nje ya nchi na kusomesha watoto wao nje.”
Sanga alibainisha kwamba hakuna mwananchi asiyependa kuishi maisha mazuri na kwamba, kitendo cha mtu mmoja kusababisha wengine kuwa maskini ni sawa na uhaini.
Naye Daud Mgaya (48), alisema mafisadi hawapaswi kupewa adhabu ya kusimamishwa kazi na kuhamisha vituo vya kazi, bali kunyogwa kwa makosa ya kuhujumu uchumi na kutaka kuwaua wananchi kwa umaskini.
“Nashangazwa na kitendo cha fisadi kuundiwa tume ya kuchuguzwa, kwani huko ni kumaliza fedha za Watanzania bila sababu za msingi,” alisema Mgaya na kuongeza:

“Naomba Katiba mpya itamke kwamba mtu akibainika kuwa fisadi hatapewa adhabu ya kusimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi, wala kuundiwa tume ya uchunguzi, au kuhamishwa kito cha kazi.”
Badala yake, Mgaya alisema fisadi apewe adhabu ya kunyongwa ili asionekani tena kulingana na kosa lake kufanana na mauaji, kwani kula fedha za wananchi ni kutaka wafe na njaa.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU