WATAKA UMEME BEI YAKE IPUNGUE ZAIDI

                                                  Makao Makuu ya Tanesco, Ubungo Dar es Salaam

WAKAZI wa Wilaya ya Kilwa, mkoani Lindi wameomba serikali kupunguza gharama za umeme unaotokana na gesi, ili kuwawezesha kumudu kutumia nishati hiyo.

Ombi hilo lilitolewa na wananchi kwenye mdahalo wa kujadili athari za mabadiliko ya tabianchi uliondaliwa na Muungano wa Asasi za Jamii Wilaya Kilwa (Kingonet).
Ali Mohamed alisema kuathirika kwa mazingira wilayani humo kunachangiwa zaidi na tabia ya baadhi ya wananchi, kushiriki upasuaji mbao na ukataji miti kwa matumizi ya kuni na mkaa kama nishati mbadala.

Mohamed alisema ni vyema serikali ikaona umuhimu wa kupunguza gharama za uunganishaji na matumizi ya umeme unaotokana na gesi asili, ili kupunguza uharibifu wa mazingira.
Naye Saidi Dege alitaka serikali kuangalia uwezekano wa kutoa elimu kwa wakulima, ili waache tabia ya kulima kandokando ya vyanzo vya maji wilayani humo.

Dege alisema iwapo serikali itatoa elimu ya kuhifadhi mazingira kwa jamii, kwa kiwango kikubwa tatizo la uharibifu wa vyanzo vya maji litapungua.

Akifungua mdahalo huo, Katibu Tawala Wilaya ya Kilwa, Simon Manjulungu aliwataka wananchi kujiepusha na uvunaji holela wa mazao ya misitu.
Manjulungu alisema mabadiliko ya tabianchi yamechangiwa pia ujenzi wa viwanda vikubwa katika nchi zilizoendelea duniani.

Awali, Mwenyekiti wa Kingonet, Elias Mwinja alisema lengo la mdahalo huo ni kusaidia kuhamasisha na kuelimisha wananchi kuhusu athari za mabadiliko ya tabianchi yaliyoanza kujitokeza hivi sasa.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

𝙂𝘼𝙈𝙊𝙉𝘿𝙄 𝙆𝘼𝘾𝙃𝙀𝙕𝘼 𝙆𝙄𝘽𝙄𝙉𝙂𝙒𝘼.