WILAYA YA MBEYA VIJIJINI - ASKARI KUMI WA JWTZ WASHIKILIWA KWA TUHUMA YA MAUAJI


[DIWANI ATHUMANI – ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.



MNAMO TAREHE 18.11.2012 MAJIRA YA SAA 23:00HRS HUKO KATIKA HOSPITALI TEULE YA IFISI WILAYA YA MBEYA VIJIJINI MKOA WA MBEYA. 


PETRO S/O SANGA,MIAKA 25,MKULIMA,MKINGA MKAZI WA CHAPAKAZI – MBALIZI ALIFARIKI DUNIA WAKATI AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU HOSPITALINI HAPO. 

MAREHEMU ALICHOMWA KISU SHINGONI NA MDOMONI NA KIKUNDI CHA WATU  WANAOSADIKIWA KUWA ASKARI WA JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA [JWTZ] KIKOSI CHA 44KJ MBALIZI TAREHE 18.11.2012 MAJIRA YA SAA 21:00HRS AKIWA KATIKA GROCERY  IITWAYO VAVENE MWE   ILIYOPO MBALIZI.

MARA BAADA YA  WATU HAO KUVAMIA BAR IITWAYO POWER NIGHT CLUB AMBAMO AWALI ALIKUWEPO PIA MAREHEMU.  

WAHALIFU HAO WALIANZA KUWASHAMBULIA WANANCHI KWA KUWAPIGA WAKITUMIA NGUMI, MATEKE, MIKANDA, MARUNGU, SIME NA MAPANGA. 

MAREHEMU  ALIJARIBU KUOKOA UHAI WAKE KWA KUKIMBIA TOKA ENEO HILO HADI   KATIKA GROSARY HIYO LAKINI WATU HAO WALIMKIMBIZA HADI ENEO HILO NA KUMJERUHI VIBAYA KWA KUMCHOMA KISU.

CHANZO CHA TUKIO HILO NI KULIPIZA KISASI KUFUATIA ASKARI GODFREY S/O MATETE,MIAKA 30,MJITA, WA KIKOSI CHA 44KJ MBALIZI KUPIGWA NA WALINZI WA KILABU CHA POMBE ZA KIENYEJI KIITWACHO DDC KILICHOPO MBALIZI  WALIOKUWA LINDONI TAREHE 17.11.2012 MAJIRA YA SAA 01:30HRS. 

BAADA YA KUSHAMBULIWA  ASKARI HUYO ALIFUNGUA KESI KITUO CHA POLISI MBALIZI USIKU HUO  KOSA – KUJERUHI NA ALIPATIWA HATI YA MATIBABU [PF3] KWA AJILI YA KWENDA KUPATA MATIBABU HOSPITALINI .

WALINZI WANNE WALIKAMATWA  KUHUSIANA NA TUKIO HILO  KWA MAHOJIANO AMBAO NI 1. FRENK S/O MTASIMWA, MIAKA 25, MHEHE 2. MURE S/O JULIAS, MIAKA 26, MMALILA 3. OMARI S/O CHARLES, MIAKA 28, MMALILA WOTE WAKAZI WA DDC MBALIZI NA 4.  LEGNARD S/O MWAMPETE, MIAKA 30, KYUSA MKAZI WA IZUMBWE. UPELELEZI WA KESI HIYO BADO UNAENDELEA.


AIDHA TAREHE 18.11.2012  WATU WENGINE SITA  WALIJERUHIWA KWA KUPIGWA SEHEMU MBALIMBALI ZA MIILI YAO  NA WANAODAIWA KUWA ASKARI WA JWTZ NA KUPATIWA HATI YA MATIBABU [PF3] KWA MATIBABU. KATI YAO WATATU WALILAZWA KATIKA HOSPITALI TEULE YA IFISI KWA MATIBABU ZAIDI. 

MAJERUHI WENGINE WATATU WALIPATIWA MATIBABU NA KURUHUSIWA. AIDHA KUFUATIA VURUGU HIZO BAADHI YA MALI ZA WATU ZILIHARIBIWA AMBAZO NI PAMOJA NA 1. GARI T.106 AWB AINA YA TOYOTA VISTA MALI YA PAULO S/O MAXIMILIAN ILIVUNJWA KIOO CHA MBELE 2. GARI T.884 AUU TOYOTA CRESTA MALI YA ALILE S/O GODFREY LILIVUNJWA SIDE MIRROR UPANDE WA KULIA. 

MWILI WA MAREHEMU ULIFANYIWA UCHUNGUZI NA DAKTARI WA SERIKALI NA KISHA KUKABIDHIWA KWA NDUGU KWA AJILI YA TARATIBU ZA MAZISHI. 

HATA HIVYO UPELELEZI WA KESI HII BADO UNAENDELEA AMBAPO JUMLA YA ASKARI KUMI [10] WA KIKOSI CHA 44KJ MBALIZI WAMEKAMATWA KUHUSIANA NA TUKIO HILO.


KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUEPUKA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI NA PINDI WANAPOTENDEWA ISIVYO HALALI NI VIZURI  KUTOA MALALAMIKO YAO KATIKA MAMLAKA HUSIKA .

VILEVILE   ANATOA RAI KWA JAMII KUJENGA TABIA YA KUTII SHERIA BILA SHURUTI. 

KAMANDA DIWANI  ANATOA POLE KWA NDUGU JAMAA NA MARAFIKI WA MAREHEMU PETRO  S/O SANGA KWA MSIBA MZITO ULIOWAKUTA NA KUWATAKA KUWA NA MOYO WA SUBIRA KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU WALICHONACHO KWANI SERIKALI, JESHI LA POLISI  LINAFANYA JITIHADA ZA DHATI KUHAKIKISHA HAKI INATENDEKA KWA  MUJIBU WA SHERIA. 

TAARIFA ZAIDI YA MATUKIO HAYA ITAENDELEA KUTOLEWA. KWA SASA HALI YA MJI WA MBALIZI NI SALAMA, WANANCHI WANAENDELEA NA SHUGHULI ZAO ZA KAWAIDA KUTAFUTA MAENDELEO.
Signed By,
                         [DIWANI ATHUMANI – ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI