YANGA YAONGOZA LIGI, SIMBA YASHANGAA BWAWA LA MINDU
Wachezaji wa Yanga pamoja na Azam wakiingia Uwanjani. (Picha zote na Habari Mseto Blog)
Benchi la Ufundi la timu ya Azam
Benchi la ufundi la timu ya Yanga
Mshambuliaji wa Yanga, Didier Kavumbagu akiipangua ngome ya Azam kabla
ya kuachia kiki kali na kuipatia timu yake bao la kwanza.
Mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva (kushoto) akichuana na beki wa
Azam, FC, Said Morad katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara
uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Yanga ilishinda 2-0.
Wachezaji wa Yanga wakishangilia
Mshambuliaji wa Yanga Hamisi Kiiza
akiwaongoza wachezaji waenzake kushangilia bao la kwanza la lililofungwa na
Didier Kavumbagu (kushoto) wakati wa mchezo wa Ligu Kuu ya Soka Tanzania Bara
uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Yanga ilishinda
2-0.
Golikipa wa Azam, Ally Mwadini akiokoa moja ya hatari zilizoelekezwa
langoni mwake wakati wa mchezo wao dhidi ya Yanga.
Kikosi cha Yanga
Kikosi cha Azam
Raha ya ushindi, hureeeeeeeeeeee
Balozi wa Fifa, Abeid Pele (wa pili
kushoto) akiwa na baadhi ya viongozi wa TFF pamoja na Mwenyekiti wa TASWA, Juma
Pinto wakati alipohudhuria mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara kati ya
Yanga na Azam FC kwenye uliuofanyika leo Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Pele yupo
nchini kwa ajili ya programu za Shirikisho
la Soka Duniani (FIFA).
MOROGORO, Tanzania
Kutoka mjini
Morogoro Simba ya jijini Dar es Salaam leo imejikuta ikiangukia pua
baada ya kuchapwa bao 2-0 na Mtibwa Sugar, mchezo litawaliwa na rabsha
za mara kwa mara kutoka kwa mashabiki wa
Simba waliokuwa na hasira wakidai mwamuzi Judith Gamba, alikuwa
hawatendei
haki.
Mtibwa
ilijipatia bao dakika ya 34, kwa bao lililofungwa na Mohamed Mkopi baada ya
Kipa Juma Kaseja kutema shuti kali la Vicent Barnabas.
Dakika
ya 87, mshambuliaji mahiri Hussein Javu, aliipatia Mtibwa bao la pili, baada ya
Kaseja kufanya mbwembwe langoni mwake.
Baada
ya mchezo kumalizika, Kaseja aliangua kilio uwanjani huku mashabiki wakimzonga.
Wachezaji wa Simba waligoma kupanda basi lao, ambako baadhi
ya viongozi wao walifanya kazi ya ziada kuwabembeleza, ambako walikubali kwa
shingo upande, lakini baada ya muda Mrisho Ngasa alishuka akiwa kabadilisha
nguo kuondoka kivyake huku akisindikizwa na mashabiki lukuki.
Yanga iliwakilishwa na
Ally Mustafa Barthez, Mbuyi Twite, Oscar Joshua, Naroub Cannavaro, Kelvin Yondani, Athuman Idd, Simon Msuva, Frank Domayo, Didier Kavumbagu, Hamis Kiiza na Haruna Niyonzima.
Azam: Mwadini Ali, Erasto Nyoni, Ibrahim Shikanda, Aggrey Morris, Said Morad, Kipre Balou, Salum Abubakar, Jabir Aziz, John Boko, Kipre Tchetche, Hamis Mcha ‘Viali’.
Comments