JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
IDARA YA HABARI (MAELEZO)
S.L.P. 9142, Dar es Salaam, Simu: 2110585, 2122771/3, Fax: 2113814, e-mail: maelezopress@yahoo.com
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Serikali
inapenda kuufahamisha umma wa Watanzania kwamba mchakato wa maandalizi
ya kutungwa kwa Sheria ya Kusimamia Vyombo vya Habari (Media Services
Bill) upo katika ngazi za juu Serikalini.
Mswada huo unatarajiwa kuwasilishwa Bungeni wakati wowote baada ya kupitishwa katika ngazi za juu za Serikali.
Mswada unaotarajiwa kuwasilishwa ni ahadi ya Serikali tangu mwaka 2007. Serikali
ipo tayari kupokea hoja mbalimbali baada ya kuwasilisha mswada huu
Bungeni kwa maana ya kuboresha ikiwemo Haki ya Kupata Habari.
Serikali
inawataka wadau wa habari na watanzania kuendelea kushirikiana na
Serikali kwa kuhakikisha kwamba Mswada wa Kusimamia vyombo vya Habari
unakamilika na kuwa sheria lengo likiwa ni kujenga misingi ya demokrasia
na utawala bora.
24/1/2013
Comments