AKUDO IMPACT 'WAZEE WA MASAUTI' KUTUMBUIZA SHINDANO LA TAIFA MISS UTALII TANZANIA 2012/13 – VIPAJI

Washiriki wa Miss Utalii Tanzania 2012/13 wakiwa katika picha ya pamoja.
Bendi ya Akudo Impact wazee wa masauti, siku ya Jumapili tarehe 17, Februari 2013, itatoa burudani katika shindano la Taifa la kumsaka Mrembo wa Utalii mwenye kipaji kati ya warembo 40 waliopo kambini Ikondelelo Lodge wakijiandaa kushiriki Fainali za Taifa za Miss Utalii Tanzania 2012/13 zitakazo fanyika mwisho wa mwezi huu katika Ukumbi wa Dar Live jijini Dar es Salaam.

Katika shindano hilo la Vipaji , ambalo litafanyika katika Ukimbi wa Jeshi wa Msasani Beach Club Jumapili kuanzia saa nane mchana ,pamoja na Bendi hiyo ya Akudo Impact , wasanii wengine watakao tumbuiza ni pamoja na mwanamuziki wa kimataifa Che Mundugwao, Msanii mdogo chipukizi wa muziki wa kizazi kipya Geneous na burudani za ngoma za asili kutoka katika kundi kongwe la Kaole  Sanaa Group wakiomgozwa na mwana dada mahili katika uchezaji wa ngoma za asili Mariam Kweji aka kalunde wa Bongo Movie.

Shindano hilo la Vipaji ni moja ya mashindano ya awali ya kuwania tuzo mbalimbali kabla ya Fainali kuu,ambapo washiriki wote watashindana kuimba na kucheza nyimbo na ngoma za makabila mbalimbali ya mikoa wanayo iwakilisha.

Mikoa hiyo na majina ya washiriki katika mabano ni  Arusha (Rose Godwin), Dar es Salaam 1 (Sophia Yusuph),Dar es Salaam 2(Ivon Stephen),Dar es Salaam 3 (Irine Thomas),Dodoma (Erica Ekibariki), Geita (Hamisa Jabiri), Iringa (Debora Jacob), Kagera 1 (Elline Bwire),  Kagera2 (Jania Abdul), Kagera 3(Mulky Uda),  Kilimanjaro (Anna Pogaly), Lindi (Joan John), Mtwara (Halima Hamis), Mara (Dorine Bukoni), Manyara (Mary C. Lita),

Wengine ni pamoja na Mbeya (Diana Joachim), Mwanza (Jesca Peter), Morogoro (Hadija Said),Tanga (Sarafina Jackson), Ruvuma 2 (Leah Makange), Tabora (Magreth Malalle), Njombe (Pauline Mgeni), Rukwa (Anganile Rogers), Katavi (Asha Ramadhani ), Simiyu (Flora Msangi), Shinyanga (Lightness Kituwa), Ruvuma (Furaha Kinyunyu), Kigoma 1(Zena Ally), Kigoma 2(Rosemary Emmanuel), Pwani (Beatrice Iddy), Singida (Neema Julius), Singida (Christina Daud),Vyuo Vikuu (Irine Richard), Vyuo Vikuu (Hawa Nyange)

Wakizungumzia kwa nyakati tofauti shindano hilo la Vipaji,Rais wa Miss Tourism Tanzania International Organisation ,wenye dhima ya kikomo ya kuandaa na kuendesha mashindano hayo , alisema kuwa mandalizi karibu yote yamekamilika kuanzia ngazi za warembo hadi burudani za bendi, ngoma za asili na muziki wa kizazi kipya.

Hili litakuwa ni tukio kubwa na la kihistoria kuwahi kufanyika Tanzania ambapo Utalii, Urembo na Utamaduni wa ngoma za asili vitaonyeshwa kwa pamoja jukwaani, lakini kivutio cha pekee ni jinsi mabinti wa kizazi kipya tena warembo kutoka mikoa yote ya Tanzania na vyuo Vikuu watakavyo onyesha maajabu ya kusakata ngoma za asili kwa umahili mkubwa na wa pekee.

Shindano la Miss Utalii Tanzania mwaka huu limedhaminiwa na wadhamini mbalimbali wakiwemo Coca Cola Kwanza Limited, Daja Salon, Mtwana Catering Services Enterprises, Zizzu Fashion, Global Publishers, Ikondelelo Lodge, Clouds Media Group, Tone Multimedia Group,Valley Spring na www.misstourismorganisation.blogspot.com

Katika Shindano hili viingilio vitakuwa ni kama ifuatavyo 5,000 kwa viti vya kawaida, 10,000 kwa V.I.P 2, na 30,000 kwa V.I.P 1 pamoja na Chakula.

Imetolewa na,
Erasto G. Chipungahelo
Rais

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU