Askofu wa Kanisa Katoliki Parokia ya Minara miwili Augustino Shao akizungumza na Waandishi wa habari kuhusiana na kuwawa kwa Padri Mushi huko Ofisini kwake Kanisa la Minara miwili.
--
ASKOFU wa kanisa katoliki jimbo la Zanzibar,Augostino Shao Alisema matukio ya uhalifu yanayoendelea kujitokeza nchini hasa kwa waumini na viongozi wa kanisa hilo hayahusiani na itikadi za kidini bali yanafanywa na watu wachache wasioitakia mema Zanzibar
Hayo yamesemwa na Askofu wa kanisa hilo Augustino Shao wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kanisa la Minara Miwili Shangani, mjini Zanzibar.
Alisema, kuongezeka kwa matukio ya uhalifu nchini, kunatokana na kutowajibika kwa watendaji wa vyombo hivyo, jambo alilosema linatoa nafasi kwa watu wenye dhamira ya kuchafua amani na utulivu uliopo nchini kutenda uhalifu.
“Matukio ya uhalifu, ubaguzi na chuki dhidi ya ukristo Zanzibar yanaendelea kushamiri kwani watu waliopewa dhamana ya kulinda na kusimamia amani na usalama wa wananchi wanaishia kukemea kwa maneno tu badala ya vitendo.pindi kunapotokea matendo hayo”, alisema Askofu Shao.
“Siwezi kuhusisha matukio haya na tofauti za dini ya kikiristo na kiislam bali ni ukosefu wa umakini kwa watendaji wa vyombo vyenye dhamnana ya kusimamia maisha ya watu.”Aliendelea kusisitiza Askofu
Hata hivyo, alisema waumini pamoja na viongozi wa kanisa hilo hapa Zanzibar wanaendelea kuishi kwa hofu na hivyo kushindwa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Aliongeza kuwa, uongozi wa kanisa hilo ulifanya juhudi za kuzungumza na watendaji wakuu wa serikali ya Zanzibar tangu lilipoanza vuguvugu la uchomaji makanisa na kufikia makubaliano ya kushirikiana katika kudhibiti hali hiyo.
Aliwataka waumini wa dini ya Kikristo na wananchi kwa ujumla kuwa wavumilivu kwa kipindi hiki cha msiba wa Padri Evaristus Mushi.
Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Aziz Mohamed, alisema jeshi hilo linaendelea na upelelezi ili kuhakikisha wahusika wa tukio hilo wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Aliwataka wananchi kushirikiana na polisi jamii kutoa taarifa zitakazosaidia jeshi hilo kukamilisha zoezi hilo kwa haraka zaidi.
“Tangu kuuwawa kwa Padri Evaristus Mushi juzi Jumapili, tuliitisha kikao cha dharura kwa maafisa mbalimbali wa Polisi, tukapeana majukumu ili kuhakikisha wahusika wanatiwa mbaroni”, alieleza kamanda huyo.
Akizungumzia suala la umiliki wa silaha nchini, alisema kwa mujibu wa sheria za Tanzania hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kumiliki silaha ya aina yoyote isipokuwa kwa kibali maalum au taratibu zinazotambulika kisheria

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI