DC - TEMEKE AWAPA NENO LA MAENDELEO WALIMU WA SEKONDARI YA JITEGEMEE MGULANI JKT

Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sophia Mjema (kulia), 
akihutubia katika sherehe za mahafali ya 19 ya Kidato
 cha sita katika Shule ya Sekondari ya Jitegemee Mgulani 
JKT Dar es Salaam leo asubuhi. Wengine ni 
walimu na wafanyakazi wa  shule hiyo. 
(Picha habari na www.mwaibale.blogspot.com)

Na Dotto Mwaibale

Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sophia Mjema, amewataka walimu  wa Shule ya Sekondari ya Jitegemee kuandika barua ya maombi kwa Manispaa ya wilaya hiyo ili wapate  viwanja vya kujenga nyumba zao kama motisha ya serikali kwao.

Mwito huo ulitolewa na Mkuu huyo wa wilaya ya Temeke wakati akizungumza na walimu hao baada ya kumalizika kwa mahafali ya 19 ya kidato cha sita ya shule hiyo Dar es Salaam leo ambapo alikuwa ni mgeni rasmi.

"Serikali inajua mazingira magumu mliyonayo hasa ninyi walimu muliopo mjini kwani hamna njia nyingine ya kujiongezea kipato" alisema Mjema.

Alisema walimu waliopo vijijini wanafursa kubwa ya kupata motisha ya kupewa mashamba na kulima hivyo kujikomboa kiuchumi tofauti na wale wa mjini.

"Nitawasaidieni katika maeneo mawili kwanza ninyi kama taasisi andike barua kuomba maombi ya kupata ardhi kwa ajili ya kufanyia shughuli zenu mbalimbali na mimi nitasaidia kulifanyia kazi jambo hilo" alisema Mjema.

Alisema katika eneo la pili kwa kila mwalimu aandike maombi ya kuomba kiwanja kwani vipo maeneo ya Kimbiji ambapo kiwanja kimoja kinauzwa sh.800 kwa mita moja.

Aliwataka walimu hao kuchangamkia fursa hiyo haraka iwezekanavyo wakati akiwa bado yupo katika wilaya hiyo kabla Rais Jakaya Kikwete haja muahamishia wilaya nyingine.

"Ningependa kuona nawasaidieni katika jambo hili kabla sijaondoka katika wilaya ya Temeke naamini mkiwa na mazingira mazuri ya kuishi  mtatoa elimu bora kwa watoto wetu" alisema Mjema.
Alisema kwamba viwanja hivyo vikipatikana na kuwa na hati miliki itasaidia kuwa dhamana ya kupata mikopo kutoka katika taasisi za fedha.

Mkuu wa Shule hiyo Luteni Kanali Martin Mkisi alitumia fursa hiyo kumshukuru mkuu huyo wa wilaya kwa kuonesha nia ya kuwasaidia walimu wa shule hiyo na kwamba mchakato huo utafanyika haraka.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.